Kuelekea katika  kipindi cha mwisho wa mwaka wasafirishaji wa abiria  pamoja na madereva hapa  hapa nchini wametakiwa kujali  ,kufuata taratibu na kanuni  na sheria za usalama barabarani  ili kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza haswa katika kipindi hichi cha kuelekea msimu wa sikukuu.

 

Hayo yamebainishwa na Afisa mawasiliano  mwandamizi wa mamlaka  ya udhibiti  usafiri Ardhini  Salum  Pazzy wakati akiongea na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonyesho ya  wiki ya nenda kwa usalama  barabarani ambayo kitaifa yanafanyikia mkoani Arusha  ambapo alisema kuwa ni vyema kila dereva ambaye anaendesha chombo  cha moto kuwa makini na kufuata  sheria za usalama barabarani kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutokuwepo kwa ajali

 

Alisema kuwa ni vyema kila dereva  akatambua amebeba roho za watu hivyo akafata sheria zote za barabarani ili kuepusha ajali kwani ajali inapotokea inapoteza roho za watu pia inapunguza nguvu kazi ya taifa .

 

“mfano dereva akaendesha gari bila kufuata sheria akawa anaendesha kwa mwendo kasi afu akapata ajali pale abiria atakapokuwa amevunjia mguu hataweza kufanya kazi tena au abiria akipoteza maisha ataweza kufanya kazi tena hivyo tutakuwa tumepoteza nguvu kazi ya taifa “alibainisha Pazzy

 

Alisema kuwa wao kama mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini katika swala zima la kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara wameanzisha  mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi ujulikanao kwa jina la (VTS)  ambao unasaidia kufatilia dereva na kujua mwendo anaoenda nao,kituo alichosimama na sehemu gari ilipo

 

Alisema kuwa mfumo huo ulianzishwa mwaka 2017 na tangu kuanzishwa  umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza ajali  za barabarani zilizokuwa zikitokea mara kwa mara haswa katika kipindi cha sikukuu hususa ni mwisho wa mwaka .

 

“ kabla ya mfumo huu watu walikuwa wameamua kuingiza hadi imani za kishirikina katika maswala ya usafiri wengine walikuwa wanasema ajali zinapotokea labda mmiliki wa chombo anatoa kafara kitu ambacho sicho cha kweli kwani ukifatilia ajali za kipindi cha nyuma asilimia kubwa madereva wake walikuwa  hawafati sheria za usalama barabarani na ndio maana ajali zilikuwa nyingi sana “Alibainisha Pazzy

 

Aidha alibainisha kuwa katika kipindi hichi cha wiki ya usalama barabarani pia wameweza kutoa eliku kwa waendesha bodaboda pamoja na pikipiki za matairi matatu (bajaji)  zaidi ya 70 ambapo wameweza kuwapatia elimu ya  jinsi ya kufuata sheria za usalama barabarani ,namna ya kufata sheria na alama za barabarani , jinsi ya kujisajili katika mfumo wa maombi ya leseni kwa njia ya mtandao pmaoja na kuwaeleza kazi za mamlaka katika sekta zinazothibitiwa.


Akiongelea mafunzo aliyoyapata katika maonyesho hayo mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Seuri Akwi alisema kuwa mafunzo hayo yamemuezesha kuelewa mambo mengi ikiwemo namna ya  kutumia alama za babarani umuhimu wa kuvaa kofia ngumu  kama abiria pia ametambua namna ya kupata leseni ya usafirishaji kutoka Latra kupitia njia ya mtandao .


Alisema kuwa ni vyema maonyesho kama haya yawepo mara kwa mara kwani yanasaidia wananchi kujua sheria mbalimbali za barabarni na kutambua haki zao wanaposafiri na hata wanapokuwa barabarani 

Share To:

Post A Comment: