Wajumbe wa baraza la wanawake wa UWT wilaya ya Makete pamoja na kamati ya utekelezaji mkoa wa Njombe wakiwa katika eneo la ukuta wa ukumbi wa UWT unaojengwa na kubomolewa na watu wasiojulikana.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Bi,Scolastika Kevela akitoa elimu ya ujasiliamali wa ufugaji wa kuku kwa wanawake wa Makete ili kujikwamua na uchumi.


 Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe inasikitishwa na vitendo vinavyofanywa na watu wasiojulikana kwa kubomoa ukuta wa ukumbi unaojengwa na Jumuiya hiyo wilaya ya Makete na kuwarudisha nyuma katika hatua za ujenzi huo.


Akizungumza na wajumbe wa baraza la wanawake wa wilaya hiyo mara baada ya kamati ya utekelezaji UWT kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,Mwenyekiti wa Jumuiya Bi,Scolastika Kevela amesema kitendo kinachofanywa na watu hao hakikubaliki kwa kuwa kimekuwa kikirudisha nyuma jitihada za maendeleo ya ujenzi.

“Tunakuja kukagua mradi tunaona watu wamebomoa,hii tumesikitika sana na huu ni uharibifu tunauita,wanamakete msikate tama”alisema Scolastika

Aidha Bi,Kevela amemuomba katibu mpya wa wilaya ya Makete Daniel Mhanza kuanza kwa kushughulikia changamoto hiyo ili kuwaondolea hofu na kukatishwa tamaa wanawake na wadau wanaojitoa katika ujenzi wa mradi.

“Huu uharibifu utakuwa mwisho baada ya kumpata huyu kamanda wetu,si dhani kama uharibifu huu utaendelea kwa kuwa huyu ni kijana na huyu anayefanya hivi atabainika na itakuwa mwisho kwa kuwa anaturudisha nyuma huu ni ushetani na siku zake zimekwisha”aliongeza Scolastika Kevela

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa wilaya ya Makete mwenyekiti wa jumuiya wa wilaya hiyo Bi,Erika Sanga ameomba kusadiwa ili jingo hilo liweze kukamilika huku akitoa rai kwa wanamakete kuendelea kushirikiana ili kufanikisha ujenzi huo utakao kuwa na tija ndani ya wilaya.

“Mimi ninachoomba kwenu wajumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa muangalie namna ya kutusaidia hili jengo ili anagalau tuliinue kwa haraka kwa kuweza kutafuta wafadili wengine anagalau tuenzeke kwasababu hali iliyopo kwa sasa ni hatari zaidi”alisema Bi,Erika

Licha ya changamoto hiyo mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda mara baada ya kutembelewa na kamati ya utekelezaji,amesema halmashauri ipo tayari kuendelea kuwasaidia wanawake katika kukuza uchumi ikiwemo kuwasaidia mikopo ili kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

“Tunataka tuwe na viwanda vidogo vidogo kwasababu malighafi zipo za kutosha lakini nani aliyeko tayari hivyo UWT mjipange huko na kwenye hili sisi tuko tayari kabisa” alisema Sweda

Kamati ya utekelezaji UWT mkoa wa Njombe imefika wilayani Makete na kukagua miradi ya jumuiya pamoja na kutoa elimu ya ujasiliamali juu ya ufugaji wa kuku kwa wanawake ili kufikia malengo yao ya kiuchumi.
Share To:

Post A Comment: