Katibu wa Kikundi cha Wabunge Vinara wa Usalama wa Chakula, Mhe Salome Makamba kushoto akiwa na wabunge vinara wa usalama na chakula wakati mkutano wa Siku mbili wa Wadau wa Lishe
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
Wabunge
Vinara wa Usalama wa Chakula wamesema kwamba watapelekea mapendelezo
Bungeni ili kuiomba Serikali iweze kuongeza kiwango cha fedha ya lishe
ya mtoto inayotengwa kila Halmashauri ya Sh.1000 kiweze kubadilishwa
badala yake wapewe kwa asilimia.
Hayo
yalisemwa leo na Katibu wa Kikundi cha Wabunge Vinara wa Usalama wa
Chakula, Mhe Salome Makamba ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Kikundi
hicho Mhe Neema Lugangira katika Mkutano wa Siku mbili wa Wadau wa
Lishe.
Mkutano huo wenye
kaulimbiu "Lishe Bora ni Msingi wa Maendeleo ya Mtaji wa Binadamu katika
Uchumi wa Kishindani" uliowakutanisha wadau wa chakula na lishe
uliofanyika jijini Tanga.
Mhe
Salome Makamba, alisema sambamba na hilo wanaomba Serikali sikivu chini
ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan iweze kuangalia upya suala la kupelekea
masuala ya chakula kusimamiwa na TBS badala yake isimamiwe na chombo
maalumu tofauti kwa sababu TBS haiwezi kuthibitisha ubora na wakati huo
huo kusimamia usalama
Katibu
huyo aliiomba pia Serikali na wadau wote wakiwemo Watanzania waweze
kusimamia suala la usafi na usalama wa chakula kwa sababu Tanzania ni
nchi Tajiri na ina rasilimali nyingi.
“Tusimamie
usalama wa chakula kutoka Shambani mpaka kwa mlaji na tuache kutupa
chakula chini lakini Halmashauri zijenge vizimba ili chakula kiwepo
mahali pa usalama na serikali iweze kusimamia kwenye masoko itasaidia
kuweza kuwa na chakula salama na safi na kutengeneza Taifa bora” Alisema
Aidha
alisema kwamba wanaipongeza Serikali kwa juhudi za kutengenza Sera,
Kanuni na Sheria mbalimbali pamoja na changamoto zote na zipo changamoto
ndogo ambazo wanaomba wafikishe ili waweze kusonga mbele kama Taifa kwa
kuweka chakula salama kwenye nchi yetu na lishe bora.
Alisema
wanaiomba Ofisi ya Waziri Mkuu iweze kukamilisha Sera ya Taifa ya
Chakula na Lishe ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwa
tarkibani miaka mitatu sasa ipo tu hapo Ofisini na inatakiwa kufanya
Maboresho ya Sera hiyo maana imeshapitwa na wakati.
Alisema
na ikibidi kabla ya hawajamaliza kipindi cha Bunge wapeleke Bungeni
mapendekezo ili iweze kutungiwa Sheria kama Sheria ya Usalama wa Chakula
huku akiipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuandaa Mpango wa Lishe kwenye
Kilimo.
Hata hivyo
aliiomba Ofisi ya Waziri Mkuu wasaidie Wizara nyengine za Kisekta ziweze
kutengeneza Mpango wa Lishe wa kisekta kama ambavyo Wizara ya Kilimo imefanya
Post A Comment: