Na Mwandishi wetu,Ngorongoro
Wagombea wa vyama Kumi na Moja katika jimbo la Ngorongoro lilipo mkoani Arusha wameteuliwa na Tume ya Taifa ya uchaguizi(NEC) kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo awali vyama 14 vilichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo lakini mpaka zoezi hilo linafungwa leo Novemba 15 saa 10:00 ni wagombea wa vyama 11 pekee ndiyo waliokuwa wamerudisha fomu zao.
Ameja wagombea hao kuwa ni pamoja na Emmanuel Shangai (CCM) Simon Bayo (SAU) Amina Mcheka (NLD) Mary Daudi (UPDP), Frida Nnko (UMD),Paulo Makuru (UDP),Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA),Simon Ngilisho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson Gagu (ACT WAZALENDO) na Zuberi Hamis (ADA TADEA).
Ametaja wagombea ambao hawakurudisha fomu ni pamoja na Singa Klekwa(CCK), Mgina Mustafa (AFD ) na Donald Laizer (TLP).
"Kwa mujibu wa ratiba ya NEC kampeni za wagombea wote zitaanza Novemba 16 mwaka huu hadi Disemba 10 mwaka huu hivyo ninaomba vyama vyote viwasilishe ratiba zao ili tuweze kuwapangia ratiba nzuri ambayo wagombea hawakutana kwenye kata moja haswa katika siku za kuzindua kampeni."Tunataka kila mgombea afanye kampeni kwa huru bila kuingiliana".
Dk,Mhina amewataka wagombea hao kufanya kampeni za kistaarabu kwa kila mgombea kunadi sera za chama chake badala ya kufanya kampeni za kupakana matope.
“Wakati wote wa kampeni naomba mtumie lugha za staha ,heshima ambazo hazidhalilishi mgombea mwingime.Shindaneni kwa sera za vyama vyenu ili kuepuka kampeni za kupakana matope''
Amesema Tume itatenda haki kwa vyama vyote ikiwa ni pamoja na kamati ya maadili ambayo itashughulikia malalamiko yote yatakayowasishwa na vyama au wagombea wanaogombea ubunge katika jimbo hilo.
Post A Comment: