Vijana 50 wa Manyoni mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika mahafali yaliyofanyika leo baada ya kuhitimu mafunzo ya ufundi yaliyogharamiwa na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt. Pius Chaya.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa mahafali hayo.
Diwani wa Viti Maalumu wa Tarafa ya Manyoni Neema Mkotya akizungumza kwa niaba ya Mbunge Dkt.Pius Chaya kwenye mahafali hayo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja.
Wahitimu hao wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.


Na Mwandishi Wetu, Manyoni


VIJANA 50 wilayani Manyoni mkoani Singida wamehitimu mafunzo ya ufundi wa fani mbalimbali kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya.

Mafunzo hayo ambayo yaligharimu Sh.51 Milioni zilizotolewa na Mbunge kutoka mfukoni mwake waliyapata katika Chuo cha Ufundi stadi (VETA) RC-MISSION Manyoni.

Fani za ufundi walizopata vijana hao ni ushonaji wa nguo, ufundi umeme wa majumbani, udereva pamoja na ufundi wa magari. 

Wakizungumza katika mahafali yao yaliyofanyika leo walisema masomo hayo yalichukua muda wa miezi tisa kwani yalianza Mwezi Februari 2021.

Gharama hizo za ufadhili huu zilitumika kulipa ada, chakula cha asubuhi, mchana na usiku, kulipia hosteli ikiwa pamoja na maji na umeme na Sare.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi, Betha Samweli alimshukuru  Mbunge Dkt Pius Chaya kwa moyo wake wa dhati wa kupenda maendeleo ya jimbo hilo kwa kuwafadhili vijana hao kwa fedha zake mwenyewe bila kutumia mfuko wa jimbo.

"Kitendo kilichofanywa na Mbunge wetu ni kitendo cha upendo ambao ameuonesha ni watu wachache mno wenye moyo wa namna hiyo wa kusaidia wenzao hasa kundi la vijana" alisema Samweli.

Kitendo alichofanya Mbunge huyo ni jambo kubwa mno kwani ameunga jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwapatia vijana ajira ambao wamekuwa na changamoto kubwa ya ajira.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: