HALMASHAURI ya Wilaya ya Ulanga imetoa Sh. 138,185,000.00 na kuvikopesha jumla ya vikundi 24 vya vijana,akina mama na walemavu wilayani hapa

Akiwakabidhi hundi yenye thamani ya fedha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amesema kuwa anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuwajali watanzania hasa kwenye mikopo isiyokuwa na riba

Malenya amesema kuwa mikopo hiyo ni ya kisheria hivyo vikundi vilivyopata mikopo hiyo vinatakiwa kurejesha kwa wakati ili nawengine waweze kupata mikopo hiyo kama ambavyo wao walivyo pewa

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri wilayani Ulanga Juma Kapilima amesema katika kuhakikisha kuwa serikali ipo chini ya jemedari Samia Suluhu Hassan mikopo hiyo kwa asilimia kubwa imetolewa kwa akina mama ukilinganishwa na akina baba  

Mbali na hilo Kapilima amewataka waliopata mikopo hiyo kuhakikisha wanasaidia katika ukusanyaji wa mapato kwa kufichua wale wote wenye tabia ya kutorosha mapato ili halmashauri iweze kukusanya fedha ya kutosha na kuendelea kutoa mikopo hiyo.

Jumla ya vikundi 24  vimekopeshwa pesa hiyo ambapo fedha yake imetoka katika vyanzo vya bakaa ya mwaka wa fedha uliopita 2020/2021  49,141,000,makusanyo ya marejesho ya mikopo kiasi cha shilingi 31,500,000,na fedha zilizotengwa kutoka asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kipindi kuanzia mwezi julai hadi septemba 2021 ni shilingi 57,544,000 na hivyo kufanya jumla ya fedha kuwa138,185,000.



Share To:

Post A Comment: