Uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini aina ya Nickel yanayosadikika kuwepo Wilayani Ngara eneo la Kabanga Mkoani Kagera, umewasili Mkoani humo Novemba 12, 2021 kwa lengo la kujitambulisha tayari kwa taratibu za kuanza shughuli za uchimbaji.
Kampuni hiyo ya Tembo Nickel yenye Makao Makuu yake Mjini London Nchini Uingereza imewasili Kagera ikiwa ni Siku chache mara baada ya kukabidhiwa Leseni Rasmi ya kuanza shughuli za uchimbaji madini hayo yanayopatikana na Wizara Yenye Dhamana.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea Wageni hao, Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, amesema hatua ya Kabanga Nickel kuwasili Mkoani Kagera kujitambulisha wakiwa pia tayari wana leseni ya uchimbaji, Ni ishara kuwa Sasa shughuli hii iliyosubirishwa kwa Takribani Miaka 40 hatimaye inakwenda kuanza.
Awali akizungumza katika Kikao hicho cha Utambulisho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera, Meneja wa Mradi huo Ndg. Benedict Busunzu amekumbusha juu ya Serikali kuwa na hisa katika Mradi huu kwa 16% wakati Kampuni ya Kabanga Nickel wakimiliki 84% na huku akizitaja hatua mbalimbali ambazo Mradi utapitia ikiwemo Kuandaa eneo ikiwemo Ujenzi wa Mgodi, Barabara, kufanya tathimini ya Wananchi watakaouguswa na Mradi, Kuchoronga mwamba, kufanya majaribio, kufanya Maandalizi ya mtambo wa uchenjuaji, na katika shughuli zote zitawahusisha wataalamu, makandarasi wanaozunguka Mradi pamoja na vibarua ambapo zaidi ya Watanzania 1000 wanatarajiwa kuajiriwa katika hatua mbalimbali.
Tayari Uongozi wa Mkoa Kagera umetoa nataka zake, na Sasa wahusika wameelekea Eneo husika kwa ajili ya mipango ya awali ili shughuli kuanza mapema, ambapo inatarajiwa zao la kwanza litapatikana baada ya Miezi 38, huku ikikadiriwa kiasi cha zaidi ya Shilingi Trioni 3 zitatumika mpaka kufikia uzalishaji.
Post A Comment: