Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa lengo la kukagua namna uongozi wa Bonde la Mto Rufiji wanavyosaidia kulinda vyanzo vya maji vinavyoingiza maji katika bwawa hilo.
Ziara hiyo imefanyika jana Novemba 13, 2021 akiambatana na Mwenyeji wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji, Mhandisi Florence Mahay.
Mhe. Mahundi amepongeza jitihada kubwa zinafanywa kuhakikisha mazingira ya Bonde la Mto Rufiji yanakuwa salama.
Aidha, ameagiza wadau wote wa maji katika maeneo yanayozunguka bwawa hilo kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu ili kuhakikisha mazingira ya vyanzo vya maji katika eneo linalozunguka mradi huo yanakuwa salama.
Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji inaunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha miradi iliyokusudiwa inakamilika kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.
Ziara ya Mhandisi Mahundi kutembelea mabonde yanayochangia maji kwenye mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ilianzia mkoa wa Njombe, Iringa, Mbeya na kuhitimishwa mkoani Morogoro.
Post A Comment: