David Ulomi
Al Hilal wamefanikiwa kufuzu hatua za makundi ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, kwa upande wa Ulomi Mafanikio hayo yanakuja ikiwa ni hivi karibuni alijiunga na Dodoma Jiji FC akitokea katika timu ya Ruvu Shooting.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 16, 2021 na Idara ya Habari na Uhusiano ya Dodoma Jiji FC imeeleza kuwa, timu hiyo imeridhia kwa kauli moja makubaliano hayo.
"Klabu yetu inapenda kuwajulisha wanahabari, mashabiki wetu na wapenzi wa soka kwa ujumla kuwa, tumefikia makubaliano ya uhamisho ya mchezaji David Richard ulomi kujiunga na Klabu ya Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu nchini Sudan.
"Klabu yetu inatoa shukurani za kipekee kwa mchezaji david Ulomi kwa mchango wake mkubwa kwenye timu yetu na tunamktakia kila lenye heri katika majukumu yake mapya," imeeleza taarifa hiyo.
Post A Comment: