Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na Maafisa na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu. Kushoto ni Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Ziwa Laurent Katakweba na Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Lusato Masinde (kulia)


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba Kijereshi na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza mara baada ya ziara yake ya kutembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiangalia mandhari ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu. Kushoto kwake ni Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Lusato Masinde.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) akizungumza na Maafisa na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu.


Baadhi ya Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba Kijereshi na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu.

*****************************

Na Happiness Shayo- WMU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka askari wa uhifadhi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa manufaa ya Taifa.

Ameyasema hayo leo katika kikao chake na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu.

“Niwaombe tufanye kazi kwa uadilifu, uwajibikaji na utii katika kulinda rasilimali za Taifa”Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, amekiagiza Kitengo cha Intelijensia kuhakikisha kinasambaratisha mitandao ya ujangili kwa kuzuia mipango yao yote na kutegua mitego ya ujangili ili kuendeleza utalii na pia ameitaka Idara ya utalii wilayani hapo kuweka mipango thabiti ya kukuza na kuendeleza utalii.

Aidha, Mhe. Masanja amewataka askari hao kushirikiana na wananchi katika kukabiliana na tatizo la tembo.

“Tuwe karibu na wananchi kwa kuwaelimisha namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu na pia inapobidi tuwapatie vifaa vitakavyowasaidia kufukuza wanyama hao ”amefafanua Mhe. Masanja.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba Kijereshi na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: