Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha Wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Bw.Daniel Ndiyo akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw.Edward Urio akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi wakiwa katika kikao cha wadau hao kujadili namna bora ya kusimamia mizigo hatarishi katika maeneo ya bandari, bandari kavu, viwanda, maghala na usafirishaji wa kemikali hizo hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.Mkemia Mkuu Dkt. Fidelis Mafumiko (katikati aliyekaa) akipata picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Rais wa Taffa Bw. Edward Urio na kulia kwake ni Mkurugenzi wa GCLA Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo.Mkemia Mkuu Dkt.Fidelice Mafumiko (katikati aliyekaa) akipata picha ya pamoja na wadau wa shughuli za usafirishaji na uhifadhi wa mizigo hatarishi zikiwemo kemikali hatarishi kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Rais wa Taffa Bw. Edward Urio na kulia kwake ni Mkurugenzi wa GCLA Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo. Mkemia Mkuu Dkt.Fidelice Mafumiko (katikati aliyekaa) akipata picha ya pamoja na wadau wa shughuli za usafirishaji na uhifadhi wa mizigo hatarishi zikiwemo kemikali hatarishi kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Rais wa Taffa Bw. Edward Urio na kulia kwake ni Mkurugenzi wa GCLA Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeandaa mwongozo wa namna bora ya kusimamia kemikali hatarishi ili kuweka utaratibu na maelekezo ya namna bora ya kusimamia mizigo hatarishi katika maeneo ya bandari, bandari kavu, viwanda, maghala na usafirishaji wa kemikali hizo hapa nchini.

Ameyasema hayo leo Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wanaoshughulika na Usimamizi wa Kemikali hatarishi uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kusimamia na kudhibiti madhara yanayoweza kusababishwa na mizigo hatarishi hasa kemikali hatarishi.

"Jitihada hizo ni pamoja na kutunga Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwanda na Majumbani, Sheria namba 3 ya mwaka 2003 na kanuni zake zilizofanyiwa mapitio mwaka 2020, ambapo Sheria hii inasimamiwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali". Amesema Dkt.Mafumiko.

Aidha amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kupitia, kujadili na kupokea maoni na mapendekezo ya kuboresha zaidi y rasimu ya mwongozo huo wa kusimamia mizigo hatarishi zikiwemo kemikali hatarishi.

Kwa upande wake rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw.Edward Urio amesema kupitia kikao hicho kitaweza kuwajengea uelewa zaidi ni jinsi gani ya kuweza kusafirisha na kuhifadhi mizigo yenye kemikali kwa manufaa ya afya za watanzania na mazingira kwa ujumla.

"Waigizaji wakubwa zaidi ya mizigo ya kemikali ni wenye viwanda na watumiaji wa usafirishaji ni wenye malori ambapo tunategemea kwenye ushiriki wao hapa wataweza kufahamu ni jinsi gani tunaweza kuhudumia hizi bidhaa hasa marighafi ya viwanda". Amesema Bw.Urio.

Amesema ni fursa kwao TAFFA kuweza kuelewa na kuwaelewesha wateja wao ambao ni nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC asilimia kubwa wanaotumia bandari ya Dar es Salaam nchi kama vile Zambia, Zimbabwe, Malawi na nyingine nyingi.

Nae Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa kampuni inayojihusisha na kupokea, kuhifadhi na kusafirisha kemilkali PMMICD Bw.Deogratius Chacha amesema semina hiyo inaenda kuwajengea uwezo wa kupokea na kuhifadhi mizigo hatarishi na kupatiwa elimu pana ambayo itawasaidia wateja ambao wanawahudumia.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: