Mwandishi wetu,Arusha


Kesi inayowakabili vigogo sita wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), imekwama kuendelea leo katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha baada ya mawakili upande wa mashtaka kushindwa kutokea mahakamani.


Kesi hiyo inawakabili vigogo sita wa mamlaka hiyo ambapo wanakabiliwa na mashtaka  ya  matumizi  mabaya ya madaraka, kula njama na kujipatia manufaa ya fedha kiasi cha Shilingi bilioni 5.3 kinyume cha sheria.


Kati ya vigogo hao waliopandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, kujibu mashtaka yanayowakabili ni aliyekuwa Mkurugenzi wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya.


Katika shauri hilo, washtakiwa ambao wapo saba mbali na Mhandisi Ruth Koya, pia yupo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiure Engineering LTD, Omari Kiure, ambaye ni mkazi wa jijini Arusha.


Washtakiwa wengine waliopanda kizimbani ni Benedict Kitigwa,James Mwambona,Steven Msenga , Godfrey Macha na Juma Mkwawa ambao wote wakiwa ni watumishi wa mamlaka hiyo ya maji AUWSA  jijini Arusha.


Akiongea mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Herieth Mtenga anayesikiliza shauri hilo wakili upande wa mashtaka,Hellen Osujaki aliiambia mahakama kwamba waendesha mashtaka wamepata dharula na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo huku akiiomba mahakama ipange tarahe nyingine.


Mara baada ya ombi hilo ndipo hakimu Mtenga aliamua kupanga kesi hiyo hadi Desemba 7 mwaka huu ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya awali.


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao, kwa pamoja walitenda makosa manne ya uhujumu uchumi na kujipatia fedha kiasi cha Shilingi bilioni 5.310,823,214 kinyume na sheria.


Watuhumiwa hao  wanadaiwa mahakamani hapo kuwa kosa la shtaka la kwanza linawahusu washtakiwa wote kwa pamoja kwa kuwa kati ya Desemba, 2017 na Oktoba mwaka 2018, katika eneo la Jiji la Arusha, washtakiwa hao walikula njama kupitia mradi wa maji wa Kanda na kujipatia manufaa isiyostahili kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Kiure Engineering LTD  bila kufuata taratibu za manunuzi.


Mwendesha mashtaka huyo, alidai kwamba shtaka la pili ni  matumizi mabaya ya madaraka na shtaka hilo linamkabili mshtakiwa wa kwanza  Mhandisi Ruth Koya, ambaye anadaiwa akiwa mtumishi wa umma na akijua kwamba ni kosa kisheria,aliiwezesha kampuni ya Kiure Engineering LTD, kupata mkataba wa ujenzi wa ofisi za Kanda za Mamlaka hiyo, kitendo hicho kilisababisha kampuni hiyo kupata manufaa ya fedha kiasi cha Sh.bilioni 5.3 kinyume cha sheria ya manunuzi ya mwaka 2011kifungu cha 36(5).


Violet, aliieleza mahakama hiyo,kwamba shtaka la tatu na la nne linamkabili mshtakiwa wa kwanza,1,2,3,4 na 5 ambao ni (Ruth Koya), mshtakiwa wa pili(Benedict Kitigwa) , mshtakiwa wa tatu(James Mwambona),mshtakiwa wan ne(Steven Msenga)  na mshtakiwa wa tano(Godfrey Macha).


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya mwezi Desemba 2017 na Oktoba 2018 wote kwa pamoja walitumia vibaya madaraka yao na kupelekwa kwa Kampuni ya Kiure Engineering LTD   kupata manufaa ya fedha kiasi cha Sh.bilioni 5.3

Share To:

Post A Comment: