Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Kituo cha haki za binadamu (LHRC) imesisitiza kuhusu mapendekezo ya Sheria zilizopitishwa ambazo hazijachukuliwa na kamati tathimini hiyo imeona kwamba mapendekezo yanayohusiana uzingatiaji wa usawa wa kijinsia Kama vile usawa kati ya wanawake na wanaume katika bodi au kamati zinazoanzishwa kisheria na mahitaji ya makundi Maalumu hayajachukuliwa.
Hayo yamezungumzwa leo na Mratibu wa mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania Hilda Dadu wakati akiwasilisha ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa kamati ya Bunge ya sheria iliyofanyika Leo jijini Dodoma.
Aidha Dadu amesema kuwa mapendekezo yaliyolenga kuishauri kamati kupunguza adhabu na kuondoa adhabu za jumla katika Sheria nayo hayakuchukuliwa
" Tunaomba na kusikitisha kamati kuangalia upya suala law adhabu za jumla pamoja na viwango vikubwa vya adhabu hizo, tunatoa wito mbele ya kamati hii kuwa utunzi wa sheria uepuke adhabu za jumla hii itawezekana endapo adhabu itokane na kifungu husika cha sheria kilichokiukwa kulingana na uzito wake" - Dadu.
Hata hivyo Dadu alimaliza kwa kusema kituo hicho kinaendelea kutuma maombi kwa kamatie na kuyapa jichoe la kipekeee na msisitizo kwa mapendekezo hayo kwa wakati ujao.
Post A Comment: