Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya yaliyojiri katika Mkutano wa 26 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika mjini Glasgow nchini Scotland hivi karibuni.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini kutekeleza maagizo ya kupanda miti 1,500,000 kila mwaka ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na kufanikisha jitihada za kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa wito huo leo alipokutana na wanahabari katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya yaliyojiri katika Mkutano wa 26 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika mjini Glasgow nchini Scotland.

Amesema Mafanikio ya mkutano huo yatadhihirika zaidi pale ambapo mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huu yatatekelezwa kwa vitendo maazimio na makubaliano yaliyofikiwa lakini zaidi utekelezaji wa mikakati ya kitaifa.

Aidha amesema waananchi wanatakiwa kuunga mkono utekelezajji wa miradi inayoendelea nchini na watendaji wa taasisi husika kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa vizuri ili kuwa na matokeo mazuri.

“Miradi ya Kimkakati ya Treni ya Umeme (SGR), Mradi wa Umeme wa Maji wa Mwalimu Nyerere na Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (BRT) imekuwa ni miradi ya mfano kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”. Amesema

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: