Afisa Maji Msaidizi  wa Bodi ya  Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji akizungumza kuhusiana na maji kupugua katika mto Ruvu wakati bonde hilo lilipofanya ziara Kibaha.

Afisa Mazingira wa Wilaya ya Kibaha Maxmillian Evarist akizungumza  kuhusiana na uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji wakati Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu ilipofanya ziara.

Ng'ombe wakiwa katika sehemu ya chanzo cha Maji Mto Ruvu katika Kidakio cha Ruvu Chini.

Shughuli za kibidamu zinazofanywa ndani ya Mto Ruvu.



BODI ya Bonde la Wami/Ruvu imefanya ukaguzi katika wakuangali upotevu wa maji  katika Mto Ruvu ili kuhakikisha maji yote yanafika kwenye vidakio ili kupunguza makali ya uhaba wa maji kwa Mikoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Katika ukaguzi huo, bonde kwa  kuaangalia mwingiliano wa shuguli za kibinadamu zinazofanywa katika Mto Ruvu  katika  Maeneo ya Mlandizi  wilayani Kibaha na kusitisha  shughuli za wafugaji na wakulima katika kipindi hiki cha uhaba wa maji.

Ukaguzi huo ni utekelezaji  wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa siku tatu kwa bonde hjilo kuhakikisha wanafatilia mwenendo wa maji kutiririka   katika mto Ruvu ambazo na kuangalia kama baadhi ya watu  wamechepusha maji hayo.

Akizungumza  katika ukaguzi Afisa Maji Msaidizi wa Bodi ya Bonde Dar es Salaam, Halima Faraji, amesema kuwa kutokana mabadiliko ya tabianchi yamesababisha  maji kapungua katika Mto Ruvu pia huku ikichangiwa na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika Mto huo.

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu  imesema inaangalia uwezekano wa kutoa maji katika Bwawa la Kidete lakini kabla ya kutoa maji hayo lazima yachunguzwe kwenye maabara kuona yanafaa kwa matumizi ya Binadamu.

Amesema bonde limekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika  kuhakikisha maji yanawafikia watumiaji.

"Kilichojitokeza sasa hivi mvua zimekuwa chache kwa mwaka huu, kumekuwa na upiungufu mkubwa wa maji ambao umeathiri Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro pamoja na Pwani, Kwa kiwango kidogo cha maji ambacho kipo kwenye Mto Ruvu tumehakikisha wananchi wanatumia maji kwa ufanisi kwa kupunguza matumizi," amesema Faraji.

Aliongeza kuwa wapo katika mpango wa kushirikiana na Wizara ya Mifugo kuhakikisha wafugaji wanajengewa mabirika na mabwawa ya kunyweshea mifugo  kwani maji katika kipindi cha kiangazi yanakuwa  madogo ili wasiingie katika mito kunywesha mifugo yao.

Aliongeza kuwa bodi itahakikisha kwa kiwango hicho cha maji kidogo kilichopo kitatumika kwa maji ya kunywa kwa wanachi mpaka pale maji yatakapoongezeka na kufanya huduma zingine  kurudi katika hali ya kawaida.      

Faraji amesema kwa hali ilipofikia kwa wale ambao hawataki kutii mamlaka watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni kulinda wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji ya kunywa.

Aidha amesema kuwa kwa wenye vibali vya kuchota maji katika mto Ruvu kuhakikisha wanapunguza viwango vyao ili maji yaende katika vidakio na kuwafikia watumiaji.

Kwa upande wa Afisa Mazingira  wa Wilaya ya Kibaha Maxmillian Evarist amesema  katika kipindi hiki cha uhaba wa maji wanaondesha shughuli kando kando ya mto Ruvu waache tu kwani kuendelea na shughuli hizo haileti afya kwa watumiaji ya maji.

Amesema wakulima wanatakiwa kubadili aina ya kilimo kwa kuacha kuvuna maji badala yake watumie 

kilimo cha  umwagiliaji wa matone ambao hautumii maji mengi kutokana na mabadiliko ya Tabaianchi.

"Jambo hili tunafanya kwa masilahi ya taifa kwa ujumla wananchi kuacha kuchepusha maji kinachotakiwa ni kuelimishana na kujengea uwezo katika kuokoa hali ya upungufu wa maji"amesema Evarist.

Amesema kuwa mabwawa yaliyotokana na Mto Ruvu bado ni sehemu ya mto hivyo kuendesha shughuli za kibinadamu kwa kudai mabwawa hayo  sio sehemu ya mto ni makosa kwani mabwawa hayo yanaweza kutumika katika kuongeza maji kwenye mto huo.

Evarist amesema hali ya Ruvu Chini ni  mbaya ukilinganisha na hali ya Ruvu juu hivyo kunahitajika nguvu zaidi na kupeana elimu ya kuweza kunusuru upatikanaji wa maji kwa wananchi wanatumia kidakio cha Ruvu chini. 


Share To:

Post A Comment: