Mkinga, TANGA 


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amesema ujenzi wa barabara ya Mkingaleo- Kinyatu hadi Bamba Mwarongo ukikamilika utafungua fursa za kibiashara katika Wilaya ya Mkinga. 


Prof. Shemdoe ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Mkinga Mkoani Tanga kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.


Akiwa katika Daraja la Mto Kinyatu lililopo katika kijiji cha Kinyatu Kata ya Mkinga amepokea taarifa ya barabara hiyo ambapo 

mkuu wa Wilaya ya Mkinga Col. Maulid Hassan Surumbu amesema barabara hiyo ambayo ni ya kimkakati   na imefungua fursa za kiuchumi kati ya kata ya Gombero tarafa ya Maramba na makao makuu ya Wilaya ya Mkinga.  


‘Barabara hii ikikamilika itawasaidia Wafanyabiashara wa samaki na dagaa wanapitisha bidhaa kwenda tarafa ya Maramba pamoja na mazao mabalimbali alisema Mhe. Col. Maulid Surumbu Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. 


Prof. Shemdoe alimwagiza meneja wa TARURA wilaya ya Mkinga kujenga ukuta wa mawe (gabion) ili kuimarisha kingo za daraja hilo. 


Aidha alitoa msisitizo kwa TARURA kuhakikisha wanapopanga ujenzi wa barabara wazipe kipaumbele barabara za kimkakati ambazo zinaenda maeneo muhimu ya uzalishaji.


Daraja hilo limejegwa kwa Tsh milion 78 fedha za mfuko wa barabara.

Share To:

Post A Comment: