Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja (katikati) akipokea mmoja wa mfuko wa saruji kati ya 200 iliyotolewa na Kampuni ya Bonanza Co.Ltd kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Hospitali ya Tumaini iliyopo wilayani humo wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki ya maendeleo ambayo kilele chake kitakuwa kuanzia Novemba 1 hadi 5.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja akipokea rangi kwenye hafla hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Ngano Limited.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Rose Kamili akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Hanang, Yohana Leonie akizungumza kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Hafla ikiendelea
Saruji na rangi iliyotolewa na wadau wa maendeleo.
Hafla ikiendelea .
Na Dotto Mwaibale, Hanang
WILAYA ya Hanang mkoani Manyara itakuwa na Wiki ya Maendeleo kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 5, 2021 ambapo utambulisho wake umefanyika mapema wiki hii katika ofisi ya mkuu wa wilaya na kuhudhuriwa na viongozi wa wilaya, Dini, Chama cha Mapinduzi (CCM) na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja amepokea saruji mifuko 200 kutoka Kampuni ya Bonanza Co.Ltd, Rangi kutoka Kampuni ya Ngano Limited, Mchanga Tripu 73 kutoka Kampuni ya HLH.
Mayanja amesisitiza makampuni yote ya kibiashara wilayanj humo kutoa sehemu ya faida kwa jamii kama sera ya ushiriki wa jamii katika majukumu inavyoelekeza kwa kuleta vifaa vya ujenzi kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 5 mwaka huu.
Mayanja amewashukuru viongozi wote wa wilaya hiyo, wadau wa maendeleo na Wananchi kwa kuliunga mkono wazo hilo na kuliboresha toka Mwezi Julai 2021 baada tu ya kuliibua.
Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja ametumia nafasi hiyo kuwaomba watu wote waliopo ndani na nje ya Hanang kushiriki kikamilifu katika wiki hiyo ili kuunga jitihada za Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuliletea Taifa maendeleo kwa vitendo.
Mayanja alisema wanategemea kupokea saruji zaidi ya mifuko 2000 ,ndoo za rangi zaidi ya 300, vigae na vifaa vingine vya ujenzi katika wiki hiyo ya maendeleo wilayani Hanang.
Post A Comment: