MKuu
wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema hadi kufikia Oktoba 14, 2021
Mkoa huo ulikuwa na jumla ya watu 19,898 waliochanjwa chanjo ya Uviko-19
aina ya Johnson.
Idadi hiyo ni sawa na 81.2 ya dozi 24,485 ya chanjo hiyo.
Sendiga
ameyasema hayo leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 ofisini kwake wakati
akizungumza na wanahabari kuhusiana na kupokea chanjo mpya ya Sinopharm.
Amesema
kuwa 0ktoba 15, 2020 Mkoa wa Iringa umepokea jumla ya dozi 21,734 za
chanjo ya Sinopharm kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Tamisemi).
"Asilimia
zaidi ya 99 ya wagonjwa ambao sasa hivi wapo katika hospitali yetu ya
mkoa ni wale ambao hawajapokea chanjo na ndio wale wanaopata maambukizi ,
kwa takwimu hizo tunaona ni uthibitisho ulio wazi kwamba unapopata
chanjo unajiweka katika nafasi nzuri,” amesema Sendiga.
Sendiga
amewashauri wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea
kuchoma chanjo ya Sinopham ambayo itatolewa kwa dozi mbili.
Kwa
upande wake mratibu wa chanjo Mkoa wa Iringa, Hans Mapunda amesema
wamepokea chanjo ya Sinopharm ambayo inatolewa dozi mbili ukilinganisha
na ile ya Johnson.
Post A Comment: