WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma wakati akiwaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza Oktoba mosi mwaka huu hadi Machi 31 mwakani.


WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma wakati akiwaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza Oktoba mosi mwaka huu hadi Machi 31 mwakani.


Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi Latifa Mohamed Khamisi,akielezea jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma wakati akizungumzia ushiriki wa maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza Oktoba mosi mwaka huu hadi Machi 31 mwakani.

.............................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amewaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza Oktoba mosi mwaka huu hadi Machi 31 mwakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 9,2021 Jijini Dodoma,Waziri Kitila amesema mwaka 2013 Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) ilichaguliwa kuwa wenyeji wa EXPO 2020 Dubai.

Amesema awali maonesho hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Oktoba mosi 2020 hadi 31,Machi 2021 lakini changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19 yalisogezwa mbele na yameanza Oktoba 2021 na yanatarajiwa kumalizika mwakani Machi 31.

Waziri Kitila amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 191 ambazo zinashiriki maonesho hayo ambapo uratibu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade).

Amesema kutokana na changamoto ya UVIKO 19 waandaaji wa EXPO 2020 Dubai wanahamasisha wafanyabiashara duniani kote kutumia fursa ya soko mtandao ambao hauna tofauti na mitandao maarufu duniani.

“Napenda kutumia fursa hii adhimu kuwajulisha na kuwaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai kupitia programu mbalimbali ambazo zimeandaliwa ikiwemo ziara za kujifunza na mikutano ya kibiashara(B2B)

Amesema programu hizo zinajikita katika teknolojia,mipango,miji na vijiji.elimu,ufundi na ubunifu,mifumo ya ufundishaji,fursa za utalii,michezo,mazingira na fukwe,usafirishaji na mawasiliano,kilimo uongezaji thamani wa mazao.

Amesema EXPO ni maonesho ya dunia yanayosimamiwa na Shirika la Kimataifa lijulikanalo kama Bureau of International Exhabition (BIE) lenye Nchi wanachama 195.

Waziri Kitila amesema waonesho hayo hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo hudumu kwa miezi sita yakiwa na kauli mbiu ya maonesho hayo ikiwa ni masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa Nchi washiriki.

Amesema Tanzania inatangaza miradi ya kimkakati kama kama vile mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP),reli ya kisasa (SGR) upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam ,ujenzi wa viwanja vya ndege na kuimarisha usafiri wa anga.

“Nchi yetu inatarajia kutumia fursa hii kubwa kushirikiana na sekta binafsi kutangaza na kutafuta mnasoko ya uhakika na endelevu ya bidhaa zinazotokana na mazao ya kimkakati kama vile kahawa korosho,chai,mkonge,karafuu,viungo,bidhaa za ngozi pamoja na bidhaa nyingine zinazokidhi mahitaji ya soko la Kimataifa,”amesema.

Waziri Kitila amesema manufaa ya kushiriki maonesho hayo ni makubwa ikiwemo kuvutia na kushawishi upatikanaji wa mitaji katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kupata wabia wa uwekezaji watakaoendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi.

Vilevile amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa makampuni kujitangaza na kunadi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini ili kupata masoko ya uhakika kimataifa.

“Maonesho haya yatatuwezesha kuvutia zaidi watalii kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini na kujifunza utamaduni na desturi za kitanzania,”amesema.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: