Afisa Mwandamizi Hifadhi ya Mwalimu Nyerere Bw.Seti Mihayom akiwa pamoja na Muhifadhi Mkuu Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Bi.Neema Mbwana wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha Maadhimisho ya kifo cha Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo hufanyika mwezi Oktoba 14 kila mwaka Afisa Mwandamizi Hifadhi ya Mwalimu Nyerere Bw.Seti Mihayo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha Maadhimisho ya kifo cha Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo hufanyika mwezi Oktoba 14 kila mwaka Muhifadhi Mkuu Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Bi.Neema Mbwana akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha Maadhimisho ya kifo cha Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo hufanyika mwezi Oktoba 14 kila mwaka
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la la hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) linawahamasisha Watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa Nyerere na Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ili kuweza kujifunza masuala mengi yanayohusu upiganiaji Uhuru na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Afisa Mwandamizi Hifadhi ya Mwalimu Nyerere Bw.Seti Mihayo amesema Hifadhi ya Taifa Nyerere ina fursa mbalimbali za uwekezaji hasa katiika shughuli za Utalii ndani ya Hifadhi hiyo.
Amesema Hifadhi ya Nyerere ina wanyama wengi wakuvutia pia ina mabwawa matano ambayo inatoa fursa kufanya utalii wa maji ambao Utalii huu kwenye maeneo ya Hifadhi ya Taifa ndio pekee wenye Utalii zaidi wa maji.
Aidha amesema Hifadhi ya Nyerere ni eneo lenye historia kubwa hasa ya Vita ya Dunia ya kwanza lakini pia na vita ya Majimaji. Na katika Hifadhi hii pia kuna eneo ambalo lilikuwa na misafara ya watumwa ililiyokuwa inapita kutokea Kilwa kuelekea Bagamoyo na Rufiji.
"Tunawahamasisha watanzania waweze kutembeelea Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ambayo ipo karibu na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo unaweza kufika kupitia barabara Kisarawe takribani kilomita 190 kwahiyo tunawahamasisha watanzania wote tarehe 14 kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere". Amesema Bw.Mihayo.
Kwa upande wake Muhifadhi Mkuu Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Bi.Neema Mbwana amesema wameandaa kampeni ambayo hasa wanadhamiria kurithisha wanafunzi urithi tulioupata kutoka kwa Mwalimu Nyerere.
"Kampeni hii imeanza toka tarehe 1 mwezi Oktoba na itaendelea kuwepo mpaka tarehe 3 mwezi Novemba. Nia hasa ya kampeni hii ni kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo historia ya upatikanaji wa Uhuru.
Amesema tayari wameshatembelea shule zaidii ya 120 kwaajili ya kuwaalika kutembelea Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ili wapate kujifunza kwa vitendo historia nzima ya upatikanaji Uhuru.
Post A Comment: