Afisa TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth Mwakatobe akiwa kwenye moja ya mikutano ya hadhara ambayo alikuwa akitoa elimu juu ya kupambana na rushwa
Afisa TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth Mwakatobe akisikilizwa na baadhi ya wananchi wakati akitoa elimu ya kupambana na rushwa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
TAASISI ya Kuzuia na
Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wilaya ya Iringa imewataka wananchi kutoa
taarifa za miradi ambayo inatekelezwa chini ya kiwango ukilinganisha na thamani
ya fedha ambazo serikali imetoa na kuwataka kuacha tabia ya kutoa na kupokea
rushwa kwa kufanya hivyo kunarudisha
nyuma shughuli za kimaendeleo kwa taifa na watu binafsi.
Akizungumza kwenye mikutano ya
hadhara ya mkuu wa wilaya ya Iringa ya kusikiliza kero za wananchi,Afisa
TAKUKURU wilaya ya Iringa Aneth
Mwakatobe alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuzilinda rasilimali za nchi
kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa
wakiwashawishi baadhi ya viongozi kutoa rushwa kwa ajili ya kufanikisha malengo
ya kinyume na taratibu ambazo zinatakiwa na wananchi wanaongoza kwa kuombwa
rushwa na baadhi ya viongozi hivyo kufanya kitendo hicho ni kosa kubwa katika
kukuza maendeleo ya nchi.
“Kuna wakati wananchi wanatoa
zawadi kwa viongozi kwa lengo la kufanikisha jambo furani bila kiongozi bila
kujua hivyo sio dhambi kutoa zawadi kwa viongozi ila inakuwa dhambi unapotoa
zawadi hiyo kwa malengo yako ambayo yanakuwa kinyume na sheria za nchi” alisema
Mwakatobe
Mwakatobe alisema kuwa taasisi
ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) inaangalia sana makosa
yanayotokana na rushwa katika jamii kwa kuwa makosa ya rushwa yapo kila kona ya
jamii hasa katika maeneo ambayo jamii inapata au inatoa huduma za kijamii.
Alisema kuwa serikali imekuwa
inatoa fedha nyingi za kimaendeleo zinaenda kufanya kazi kwenye vijiji na mitaa
ambayo kwa kiasi kikubwa inawalenga wananchi wa maeneo husika hivyo kila
mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa miradi ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao
kwa kuwa miradi hiyo ni mara ya wananchi.
“Miradi yote inayoletwa kwenye
maeneo yenu ni mali yenu hivyo mnapaswa kuilinda na kuhakikisha miradi yote
inatekelezwa kulingana na thamani ya fedha ambayo inakuwa imetolewa na
serilikali kwenye mradi husika” alisema Mwakatobe
Mwakatobe alisema kuwa bila kuisimamia
vilivyo miradi hiyo basi serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi bila mafanikio
yanayotarajiwa hivyo wananchi wanajukumu la kuhakikisha wanasimamia jukumu hilo
kikamilifu ili miradi itekelezwe kama inavyotakiwa.
Aliwaomba wananchi wa wialaya
ya Iringa kutoa taarifa pale ambapo wanahisi kunaharufu ya rushwa kwa kupiga
bure namba ya simu ya 113 ambayo itawasaidia taasisi hiyo kupata taarifa hizo
na kuanza kuzifanyia kazi mara moja.
Alimazia kwa kuwataka wananchi kuikata rushwa kwa kuacha tabia ya kutoa rushwa,kuwashawishika kupokea rushwa hapo ndio Tanzania itapata maendeleo yanayotakiwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Post A Comment: