Taasisi ya Maryprsca Women Empowerment Foundation(MWEF) imechangia shilingi laki tano kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu cha tatu cha Padre Benedict Mwamlima kiitwacho"Shinda Mfadhaiko"uzinduzi uliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Parokia ya Kyela Mjini mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Ismail Mlawa.
Akiiwakilisha Taasisi hiyo katika ibada Adam Simbaya amesema kwa niaba ya Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) amesema lengo ni kumuunga mkono Padre Mwamlima kwa ajili ya kuelimisha jamii.
Paroko Leonce Pesambili amesema jamii inapaswa kumuunga mkono Padre Mwamlima ili aendelee kutunga vitabu.
Katika risala iliyosomwa na Audiface Temba imesema jumla ya shilingi milioni kumi zinahitajika kuchapisha nakala za vitabu na kuvisambaza.
Aidha Katibu wa Mbunge Miriam William amesema lengo la kutoa mchango huo vitabu viweze kuwafikia wanawake hususani wajane ili nao wanufaike na ujumbe ulipo katika vitabu.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Ismail Mlawa amewataka Watanzania kuwa na tabia za kusoma vitabu kwani ndani yake kuna maarifa mengi.
Post A Comment: