Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
Ndalichako akikata utepe kuashiria kuanza kwa uzinduzi wa zoezi la
usambazaji wa vitabu vya Kiada Shule za Msingi na Sekondari
vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania,vitabu hivyo vitasambazwa
katika halmashauri zote 184 nchini
Mkuu
wa kikosi 95 kikosi cha usafirishaji JWTZ,Kanali Benjamini Kisinda
akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari namna watakavyosambaza
vitabu hivyo nchi nzima
Baadhi ya Magari ya JWTZ yatakayotumika kusambaza vitabu hivyo nchi nzima
Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
Ndalichako sambamba na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wakiwasili kwenye hafla fupi ya
uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vitabu vya Kiada Shule za Msingi na
Sekondari vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania,vitabu hivyo
vitasambazwa katika halmashauri zote 184 nchini.Pichani kulia ni
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba na kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Gerald Geofrey Mweli
Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
Ndalichako akiwapungia mkono Wageni waalikwa mbalimbali wakati akielekea
kukagua ghala la vitabu,ambapo zoezi la uzinduzi wa usambazaji wa
vitabu hivyo vya Kiada Shule za Msingi na Sekondari vilivyoandaliwa na
Taasisi ya Elimu Tanzania umeanza leo .
Pichani
kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa
Joyce akieleza jambo kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini
Dkt.Aneth Komba wakati akiendelea kukagua vitabu vilivyomo ndani ya
ghala hilo,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akishuhudia
Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
akimuonesha jambo kwenye moja ya kitabu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,pichani kulia ni Mkurugenzi
mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akishuhudia
Pichani
kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa
Joyce akieleza jambo kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini
Dkt.Aneth Komba wakati akiendelea kukagua vitabu vilivyomo ndani ya
ghala hilo,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na pichani kati ni Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
anayeshughulikia masuala ya Elimu Gerald Geofrey Mweli
Sehemu ya vitabu ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika halmashauri zote 184 nchini
Mkurugenzi
mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akimueleza jambo Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
Mgeni
rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce sambamba
na Wageni wa Meza Kuu wakitoka ndani ya ghala mara baada ya kushuhudia
shehena ya vitabu vya Shule ya Msingin na Sekondari vinavyotarajiwa
kuanza kusambazwa leo nchi nzima
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia tukio hilo
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya elimu nchini imetumia shilingi Bilioni 46.476 kwa ajili ya kuchapa vitabu nakala 20,943,989 vya elimu kuanzia ngazi ya Awali,Msingi,Kundirika,Maandishi yaliyokuzwa pamoja na Sekondari.
"Wizara itaendelea kusimamia kila pesa inayoletwa na Serikali katika kuendeleza Elimu nchini hivyo napenda kutoa shukrani zangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mhe.Samia Suluhu kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu"alisema Mhe.Ndalichako.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt Aneth Komba amesema kuwa vitabu hivyo vimeandaliwa na wataalamu wa TET kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka vyuo vikuu, vyuo vya Ualimu pamoja na walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi.
Zoezi la usambazaji wa vitabu hivyo limeanza leo mara tu baada ya uzinduzi.
Post A Comment: