Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Waandishi wa Habari.
Serikali ya Tanzania imepiga
marufuku utengenezaji na uwekaji wa Plastiki laini kwenye mifuniko ya
chupa za maji (viremba vya juu) ikiwa pamoja na mirija ya Plastiki
inayotumika katika vivywaji hivyo, katika kipindi cha miezi sita baada
ya katazo hilo kuanzia Oktoba 11, 2021.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, Mhe. Selemani Jafo amesema katazo hilo limekuja baada ya
kuwepo kwa athari za mazingira kwenye mazalia ya Samaki, Wanyama
mbalimbali kutokana na Plastiki hizo kuenea kwenye nyasi, mifereji na
vyanzo vingine vya Maji.
Jafo
amesema kulingana na Kifungu cha Sheria ya nchi No. 13(2), Sheria No.
20 ya Sheria ya Mazingira, 2004 ametoa maelekezo ya kupiga marufuku hiyo
ya kuweka Plastiki laini kwenye bidhaa hizo hapa nchini na bidhaa
zinazozalishwa nje ya nchi.
“Baada ya miezi Sita hatutarajii
kuona bidhaa hizo zinazalishwa zikiwa na karatasi laini juu ya mifuniko,
lazima tulinde mazingira yetu yanayotuzunguka”, amesema Jafo.
Amesema
baada ya miezi Sita kuisha, Wazalishaji na Wasambazaji wa bidhaa hizo
wanaelekezwa kuzalisha bidhaa zao bila kuweka Plastiki laini nje ya
Chupa hizo.
Post A Comment: