Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na tabasamu baada ya kukagua miradi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakizungumza mara baada ya ziara
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na  mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakikagua miradi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa 
Mmoja ya majengo yanayojengwa katika kituo cha afya Isman ambayo kwa ujumla wake yanatakiwa kujengwa majengo matano


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhakikisha inasimamia vilivyo miradi inayokelezwa katika Halmashauri hiyo ili kuendana na thamani ya fedha ambazo zinakuwa zimetolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii katika maeneo husika.

 

Akizungumza wakati wa kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo,mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa imebahatika kuwa na miradi mingi ya kimaendeleo ambayo imetumia mamilioni ya fedha kutoka serikalini kuu na serikali za mitaa kwa ajili ya kukuza maendeleo ya wananchi.

 

Sendiga alisema kuwa miradi aliyoitembelea kwa siku ya leo kwa kiasi kikubwa imetekelezwa katika ubora ambao unatakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolea kwenye mradi husika kama vile ujenzi wa majengo matano ya kituo cha afya cha Ismani,ujunzi wa vyumba viwili ya shule ya sekondari ya Nyang’oro na Lyandembela.

 

Alisema kuwa amefurahishwa kwa namna ambavyo miradi yote hiyo imejengwa kwa ubora hasa miradi ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Nyang’oro na Lyandembela na ujenzi unaondelea katika kituo cha afya cha Ismani alilidhishwa na ubora wa vifaa vya ujenzi vinavyotumika kujengea kama vile tofali zenye ubora unaotakiwa,saruji ilivyochanganywa kwenye ubora unaotakiwa.

 

Sendiga aliwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kusimamia vizuri miradi yote inayotekelezwa ambayo imekuwa inaubora unaotakiwa kulinga na thamani ya fedha ambazo zimetolewa na serikali.

 

Alisema kuwa uongozi wa wilaya na halmashauri wamefanya kazi kubwa kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwenye ubora unaotakiwa kama ambavyo serikali inataka kujengwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa ajili ya jamii.

 

Aidha sendiga alisema kuwa hajaridhishwa na fundi aliyepewa kazi ya kutengeneza madawati ya shule ya sekondari ya Nyang’oro chini ya kiwango na kupelekea kuharibika kabla ya kuanza kutumika hivyo kumuamuru fundi huyo kutengeneza tena madawati hayo kwa gharama zake.

 

Alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuhakikisha anamsimamia fundi huyo anatengeneza madawati hayo kwenye ubora unaotakiwa kama ambavyo madawati mengine kwenye shule hiyo yalivyotengenezwa na kudumu kwa miaka mingi.

 

Mkuu wa mkoa huyo alifanikiwa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa majengo matano ya kituo cha afya cha Ismani na kuzindua vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Lyandembela iliyopo katika kata ya Ifunda.

 

Sendiga alimazia kwa kuwapongeza viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa na kusababisha kuleta matokeo chanya kwenye miradi ambayo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.

 

Alisema kuwa anawapongeza wananchi wote ambao wamekuwa wanajitokeza kuchangia nguvu zao kwenye miradi yote ambayo imekuwa inayotekelezwa kwenye maeneo yao na kuipatia nguvu serikali kuendelea kupeleka miradi kwenye halmashauri hiyo

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhuru Hassan ametoa kiasi cha shilingi Milioni Mitatu (300,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura na ametoa shilingi milioni mia nne na ishirini (420,000,000/=) kwa ajili ya mashine ya mionzi (exrey).

 

Alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhuru Hassan kwa kuwapatia fedha hizo ambazo zikifika zitafanyiwa kazi kwa haraka sana na kwenye ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha hizo.

 

Moyo alisema kuwa hata mvumia mtu yeyote yule ambaye atakuwa anaihujumu miradi ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa katika wilaya ya Iringa hivyo miradi yote itatekelezwa kulingana na thamani ya fedha ambazo ambayo itakuwa imetolewa na serikali kwa ajili ya mradi husika.

 

Alisema kuwa tatizo la maji katika tafara ya Isiman litatuliwa  na mradi wa maji wa Kilolo na Isman ndio utakuwa suruhisho la kupatikana kwa maji na kumaliza changamoto zote ambazo zinapatika na kukosekana kwa maji.

 

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bashir Muhoja alisema kuwa walipokea kiasi cha shilingi milioni mia nne (400,000,00/=) kwa ajili ya majengo matano ambayo ni jengo la Maabara,nyumba ya mtumishi wa kituo hicho,jengo la kuhifadhia maiti,jengo la upasuaji na jengo wazazi

 

Alisema kuwa katika ujenzi wa majengo hayo matano wameshatumia kiasi cha shilingi milioni mia mbili sabini na sita (276,000,000/=) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya viwandani kama vile saruji,malumalu,vifaa vya mbao,nondo, Gypsum Board na vifaa vingine vinavyohitajika katika ujenzi huo.

 

Muhoja alisema kuwa mradi huo umekumbana na baadhi ya changamoto kutokana na kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi sokoni kama vile vifaa vya vyuma na kusema kuwa kiasi cha shilingi milioni mia nne (400,000,00/=) haziwezi kukamilisha kituo hicho.

 

Alisema kuwa fedha iliyo inaweza kufikisha asilimia 95 na kutakosekana baadhi ya vitu vitakosekana  ambavyo vitasababisha kutofikia lengo la kumaliza majengo hayo na kuanza kutumika kama inavyotarajiwa na serikali.

 

MWISHO.

Share To:

Post A Comment: