Nteghenjwa Hosseah, Arusha


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhi hundi  yenye thamani ya Sh 1,396,817,375 kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu.


Rais Samia amekabidhi hundi hiyo mapema leo wakati akizindua Hospitali ya Jiji la Arusha katika eneo la Njiro kata ya Engutoto jijini Arusha.


Kiasi hicho cha fedha kinachokwenda kunufaisha vikundi 150, takribani Sh milioni 532 zimetokana na  mapato ya ndani ya halmashauri wakati Sh 848 ni zile zilizotokana na  marejesho ya mikopo ya nyuma.


Fedha hizo zinakwenda kunufaisha vikundi 106 vya wanawake vilivyotengewa Sh milioni 896, vikundi 36 vya vijana  vitapata Sh milioni 445 na vikundi 8 vya watu wenye ulemavu vitakavyopewa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 41.


Utoaji wa hundi hiyo leo unaifanya Jiji la Arusha kuwa kinara Kitaifa kwa kutoa mikopo yenye thamani ya  Sh bilioni 3.5 ndani ya miezi saba ya kipindi cha Uongozi Serikali ya Awamu ya Sita.


Wakati huo huo Rais Samia amezindua ubao wa mikopo (Dash Board) utakaoonyesha taarifa zote muhimu kuhusu mikopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Share To:

Post A Comment: