MTENDAJI Mkuu wa kampuni ya Puma Energy ukanda wa Afrika Fadi Mitri amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ushirikiano katika kuendeleza uchumi wa Tanzania kupitia kampuni hiyo na bidhaa zake.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vilainishi vipya vya Puma leo jijini Dar es Salaam Mitri amesema, Kampuni hiyo ina malengo ya kuifikia jamii na kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa mafuta na vilainishi kwa gharama nafuu, kiwango sahihi na ubora wa kiwango cha juu na wamekuwa wakishirikiana na serikali katika kuhakikisha kupitia Puma Energy na bidhaa zake uchumi wa taifa unakuwa imara na wenye tija kwa jamii
Amesema katika kufanikisha hilo, Puma Energy itawekeza zaidi ya dola milioni 100 sawa na shilingi bilioni 230 za Tanzania kwa miaka mitatu ijayo nchini Tanzania na uwekezaji huo ni kwa malengo ya kuifikia jamii na wateja wao kupitia huduma zao.
''Tungependa kuwaalika wateja wa thamani kubadili machaguo na kwa sasa waichague Oil na vilainishi chapa Puma Energy vyenye ulinzi wa uhakika kwa injini, ubunifu wa vifungashio na teknolojia ya juu katika utengenezaji wa bidhaa zetu.'' Amesema.
Aidha amesema, Puma Energy wapo makini katika kuhakikisha wateja wao wanapata bidhaa halisi zenye viwango vya hali ya juu na kwa kuzingatia usalama, gharama nafuu na upatikanaji wa uhakika kote nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema kampuni hiyo imewekeza muda katika kutafuta namna bora zaidi ya kuboresha bidhaa na huduma zao.
'' Puma ni kampuni ya Serikali na watanzania, Leo hii tumewaletea vilainishi vyenye ubora katika soko la Tanzania vyenye kukidhi vyombo vyote vya moto na vyenye ubora wa juu na niwashauri watumiaji wa vyombo vya moto, viwanda, shughuli za ujenzi ikiwemo reli na migodi kuchagua vilainishi vya Puma ambavyo vimetengenezwa na kuratibiwa nchini Uswisi kwa kuzingatia matakwa na ubora wa viwango vya taifa na dunia kwa ujumla.'' Amesema.
Awali akifafanua kuhusu upekee na ubora wa vilainishi hivyo Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Prosper Kasenegala ameeleza kuwa vilainishi hivyo ni halisi visivyoweza kughushiwa na vinakidhi mazingira ya Tanzania katika vyombo vya moto, na mashine katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, kilimo, ujenzi na katika migodi.
Amesema, vilainishi hivyo vya Puma Energy vinapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Puma Energy muda wowote, katika ubora wa hali ya juu na kwa gharama nafuu.
Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri (katikati) akikata utepe wakati wa kuzindua bidhaa mpya ya vilainishi chapa Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah.Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Fadi Mitri akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan Ushirikiano katika kujenga uchumi. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy na kueleza kuwa Puma Energy hawalali, wamewekeza muda wao katika kuboresha huduma na bidhaa zao, hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Prosper Kasenegala akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy na kueleza kuwavilainishi hivyo vinapatikana katika vituo vyote vya mafutakote nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Post A Comment: