Jane Edward, Arusha
Shirika la nyumba la Taifa (NHC) limewaasa wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za nyumba bora na za kisasa zinazoendana na viwango vya sasa zilizopo katika shirika hilo wakati nyingine zikiendelea kujengwa hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Afisa mwandamizi wa mauzo na masoko kutoka shirika hilo,Tuntufye Mwambusi wakati akizungumzia fursa mbalimbali zilizopo katika shirika hilo ambapo kuwa, kwa mkoa wa Arusha wana mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi katika mji wa Safari City eneo la Kisongo ambapo nyumba hizo zimepangwa vizuri huku zikiwepo huduma zote muhimu
Amesema wameweza kujenga nyumba za mfano na nyingine waliuza kwani wana punguzo la asilimia 40 kwa sasa hivi ,hivyo aliwataka wananchi katika mikoa mbalimbali kuchanganya fursa hiyo .
Ameongeza kuwa,wameleta mradi huo wa Safari City kwa sababu wanaelewa changamoto ya mipango miji katika jiji la Arusha ,hivyo wakaamua kuja na mradi huo ambao ni mfano wa kuigwa kwani umepangwa vizuri huku huduma zote za kijamii zikipatikana kwa urahisi.
Tuntufye amebainisha kuwa, wana mradi wa ujenzi wa nyumba Dodoma ambapo wanajenga makazi elfu Moja na wanatarajia kuzindua hivi karibu huku akisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu Sana na Serikali na wataweza kuuza hizo nyumba pia.
“Kwa mkoa wa Arusha hapa mtu unaweza kuweka uwekezaji mkubwa kwani Kuna fursa kubwa Sana za kibiashara ndio maana na sisi tunaendelea kuwekeza zaidi ili kuwarahisishia huduma wateja wetu na kuwaletea huduma kwa karibu zaidi.”amesema
Aidha Tuntufye aliwataka watanzania watumie fursa katika kuchukua nyumba hizo za shirika la nyumba zilizopo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuweza kupata huduma nzuri .
Post A Comment: