NAIBU
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ametoa Siku
14 kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuhakisha
kuwa anafamy uhakiki wa madeni yote ya watumishi na kuyawasilisha Ofisi
ya Rais Utumishi ili waweze kulipwa haki yao wanayoistahili.
Ndejembi
ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Manispaa hiyo kwa ajili ya
kuzungumza na watumishi wa umma lengo likiwa kuwasikiliza changamoto zao
na kuzitatua papo kwa papo.
Akijibu changamoto hiyo ya
malimbikizo ya mishahara ambayo wanadai watumishi hao, Naibu Waziri
Ndejembi amesema Wizara ya Utumishi imekua ikilipa madeni hayo kwa
haraka pindi ambapo wamekua wakiletewa orodha ya watumishi wanaodai na
kwamba watumishi wanapoona wamechelewa kulipwa wajue shida haipo
wizarani bali ipo kwa Maafisa Utumishi kwani wao ndio wamekua
wakichelewesha upelekaji wa majina.
"Natoa siku 14 mpaka ifikapo
Oktoba 22 Afisa Utumishi wa Manispaa ya Songea na wengine wote nchini
sisi Ofisi ya Rais Utumishi tuwe tumepata madeni ya watumishi wote wa
Manispaa ya Songea wanaostahili kulipwa ili tuweze kuyafanyia uhakiki
yaweze kurudishwa,Sisi Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajali
watumishi wake hivyo tuleteeni majina tuyahakiki na kuyapeleka Hazina
ili waweze kulipwa wote haki yao.
Maafisa Utumishi harakisheni
kufanya uhakiki na kutuletea orodha hizo, hizi ni haki za watumishi wetu
siyo hisani ni jasho lao hivyo wanapaswa kulipwa stahiki zao, na nitoe
wito pia Kwa Watumishi wote wenye kudai fuatilieni majina yenu kwa
Maafisa Utumishi ili ndani ya hizo wiki mbili nilizotoa tuweze kupata
orodha yenu na kuifanyia kazi," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.
Akijibu
changamoto ya watumishi wa umma waliopandishwa madaraja mwaka 2016 hadi
2017 na kisha baadaye kuondolewa madaraja hayo, Naibu Waziri Ndejembi
amesema hakuna mtumishi wa umma aliyepanda daraja kwa kipindi hicho
kwani baadaye walitumiwa tena barua za kufuta madaraja hayo.
"Naomba
ieleweke baada ya kutumiwa barua za kupandishwa madaraja katika kipindi
hicho cha 2016 na 2017 baadaye walitumiwa tena barua za kufuta madaraja
hayo kwa kuwa Serikali ilihitaji kufanya uhakiki lakini baada ya
uhakiki Novemba 2017 tulianza kupandisha tena madaraja hivyo niwaombe
mtambue hakuna daraja linaloitwa Daraja la Mei 2016 lilishaondolewa kwa
agizo la Serikali.
Katika kutambua umuhimu wa watumishi wetu wa
umma bajeti ya upandishaji madaraja kwa watumishi mwaka huu ilikua
tupandishe watumishi 91,000 tu lakini kwa upendo wa Rais Samia kwenu
watumishi alitoa maelekezo kuwa tupandishe yeyote ambaye anastahili
kupanda daraja mwaka huu na hivyo tumepandisha mpaka Sasa 174,000 hivyo
tumekwenda mara mbili ya bajeti iliyokua imepangwa, tumpongeze Rais
wetu," Amesema Ndejembi.
Naibu Waziri Ndejembi pia ametoa wito
kwa Watumishi wa umma nchini kuchukua tahadhari za ugonjwa wa UVIKO-19
ikiwa ni pamoja na kuchoma chanjo kama ambavyo Rais Samia amekua
akishauri na kuwataka kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi madhara
ya ugonjwa huo na kuwashauri kujitokeza kwa wingi kuchoma chanjo ili
kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
Home
Unlabelled
NAIBU WAZIRI NDEJEMBI ATOLEA UFAFANUZI UPANDISHWAJI WA MADARAJA YA WATUMISHI WA UMMA
Post A Comment: