Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali imeendelea
kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji la Mwanza
lengo ikiwa ni kuboresha zaidi mkoa huo ambao unashika nafasi ya pili
kwa kuiingiza nchi mapato nyuma ya Dar es Salaam, ameyasema hayo leo
Oktoba 17, 2021 wakati akitoa taarifa ya wiki ya Serikali akiwa jijini
Mwanza.
”Mwanza ni
Mkoa wa pili nchini kuchangia fedha nyingi katika pato la Taifa, mwaka
2019 makusanyo ya mapato yalikuwa Sh Trilioni 10.2 na hivyo kuchangia
Pato la Taifa kwa 7.35% na mwaka 2020 yalikuwa Trilioni 10.9 hivyo
kuchangia Pato la Taifa kwa 7.38.8%,” ameeleza Gerson Msigwa, Msemaji
Mkuu wa Serikali.
Ametaja
moja ya miradi mikubwa jijini humo ni soko kuu la kisasa linaloendelea
kujengwa. ”Tunajenga Soko la Kisasa Mjini ambapo zimeshaletwa Sh Bilioni
8, hadi kukamilika utagharimu Bilioni 20.3, zimeletwa Bilioni 4.5 kwa
ajili ya ujenzi wa Jengo la Abiria kwenye uwanja wa Mwanza ambapo ujenzi
ukikamilika utagharimu Shilingi Bilioni 13.3”.
Post A Comment: