Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (wa
pili kushoto) akikabidhi sehemu ya vyakula vyenye thamani ya shilingi
Milioni 1.6 kwa ajili ya mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni
wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy amekabidhi
vyakula vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya mabinti
waathirika wa ndoa na mimba za utotoni wanaosoma katika shule ya
Sekondari ya Agape Knowledge Open School ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Kike duniani.
Akizungumza
leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 wakati wa kukabidhi vyakula hivyo katika
shule ya Agape Knowledge Open School iliyopo katika mtaa wa Busambilo
kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga, Munissy amelishukuru shirika lisilo
la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) kwa kuendelea
kuwasaidia na kulea mabinti hao waliopata changamoto za ukatili wa
kijinsia.
“Sisi
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni wadau wa haki za mtoto wa kike na
baadhi ya mabinti waliopo kwenye shule ya Agape wanatoka Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga, hivyo katika kusherehekea Siku ya Mtoto wa kike
duniani ambayo hufanyika Oktoba 11 tumeamua kuja hapa ili kuwapatia
chakula”,amesema Munissy.
“Tumeleta
mchele kilo 500, maharage kilo 500, lita 40 za mafuta ya kupikia na
chumvi vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 1,690,000/= ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Siku ya mtoto wa kike mwaka huu 2021”,ameongeza
Munissy.
Aidha
amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la Agape na
mashirika mengine ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kumlinda mtoto
wa kike na kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi
huyo wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga amewataka mabinti hao kusoma
kwa bidii na kutokubali kurudi nyuma ili waweze kutimiza ndoto zao huku
akiwaomba kuwa mabalozi wazuri katika jamii kueleza madhara ya matukio
ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Sitegemei
kuona wala kusikia binti aliyepo katika shule hii anapata mimba au
kukatisha masomo na kuolewa, someni kwa bidii huku mkijishughulisha na
ujasiriamali,fanyeni kazi za ubunifu ambazo zitawaingizia
kipato”,amesema Munissy.
Katika
hatua nyingine ameitaka jamii kuachana na vitendo vya kuozesha watoto
wadogo kwani kufanya hivyo ni ukatili hivyo wawapeleke shule na
kuwapatia mahitaji muhimu ili waweze kutimiza ndoto zao na kwa wale
wanaoendekeza vitendo vya ukatili wa kijinsia watachukuliwa hatua za
kisheria.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape AIDS Control Programme
(AACP),linalomiliki shule hiyo,John Myola ameishukuru Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga kwa msaada huo wa chakula kwa ajili ya wanafunzi wa
kike.
“Tunawashukuru
sana Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa kutupatia chakula kwa ajili
ya watoto wetu hawa ambao ni waathirika wa matukio ya ukatili wa
kijinsia, tunawashukuru sana kwani mmekuwa wadau wazuri, mmekuwa
mkitusaidia mara kwa mara hiyo ni kuonesha kwa vitendo kuwa hawa watoto
ni wetu sote”,amesema Myola.
Myola
amesema hivi sasa katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open
School iliyoanzishwa mwaka 2014 , sasa wana jumla ya wanafunzi 48 na
tangu mwaka 2017 ufaulu wa wanafunzi wa kidato umekuwa mzuri wana uwezo
mkubwa darasani ambapo baadhi yao wamejiunga na masomo ya kidato cha
tano na wengine vyuo mbalimbali.
Amesela
Uwepo wa watoto yatima na waathirika wa ndoa na mimba za utotoni ndiyo
ulisababisha shirika la Agape kuanzisha kituo cha elimu ya sekondari
cha Agape Knowledge Open School.
Hata
hivyo Myola amesema bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya miundo
mbinu ya madarasa hivyo kuwaomba wadau kujitokeza kusaidia shule hiyo
ili wanafunzi wawe katika mazingira rafiki zaidi.
Kwa
upande wao wanafunzi hao wameishukuru Halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga kwa kuwapatia chakula huku wakieleza kuwa elimu wanayoipata
imewajengea uwezo mzuri wa kujitambua,kufikiri,kufanya maamuzi sahihi na
mambo kadha wa kadha ikiwemo elimu ya ujasiriamali,stadi za maisha na
stadi za kazi na afya ya uzazi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akizungumza
leo Jumamosi Oktoba 16,2021 wakati akikabidhi vyakula vyenye thamani ya
shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya mabinti waathirika wa ndoa na mimba
za utotoni wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open
School ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike duniani. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akizungumza
wakati akikabidhi vyakula vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 kwa
ajili ya mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni wanaosoma katika
shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Shirika la Agape, John Myola, kulia ni Mkuu wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP), linalomiliki ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School ,John Myola akizungumza wakati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (katikati)
akikabidhi vyakula vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya
mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni wanaosoma katika shule
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akizungumza wakati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (katikati)
akikabidhi vyakula vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya
mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni wanaosoma katika shule ya
Sekondari ya Agape Knowledge Open School.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (wa
pili kushoto) akikabidhi sehemu ya vyakula vyenye thamani ya shilingi
Milioni 1.6 kwa ajili ya mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni
wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School. Wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja. Wa kwanza kulia ni Afisa
Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bi. Aisha Omary
akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape, John Myola na
mmoja wa wanafunzi 48 wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School

Sehemu
ya vyakula kwa ajili ya mabinti waathirika wa ndoa na mimba za utotoni
wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School
vilivyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP), linalomiliki ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School ,John Myola wakati akitembelea Maktaba ya shule hiyo alipowasili kukabidhi vyakula kwa ajili ya wanafunzi wa kike shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP), linalomiliki ya Sekondari ya Agape Knowledge Open School ,John Myola wakati akitembelea madarasa ya shule hiyo alipowasili kukabidhi vyakula kwa ajili ya wanafunzi wa kike shuleni hapo.

Post A Comment: