********************************
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) ameuhakikishia ujumbe wa wafanyabiashara, wawekezaji na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa Czech kuwa Tanzania iko tayari kuwapokea kuja kuwekeza Tanzania kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Waziri Mkumbo ameyasema hayo alipokutana na Ujumbe huo ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Czech Mhe. Miloslav Stasek pamoja na Mhe. Martn Klepetko Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Mhe. Krel Tyll Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Czeck leo 07/10/2021 jijini Dar es salaam.
Prof. Mkumbo aliueleza ujumbe huo ulioko utayari kiwekeza na kufanya biashara Tanzania katika Sekta ya anga, Ujenzi wa Mitaa ya viwanda, Kilimo na mengineyo kuwa utayari wa nchi unachochewa na dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inajikita katika uchumi wa viwanda.
Alifafanua zaidi kuwa Serikali imefanya jitihada kubwa mbalimbali ikiwemo kufanyia marekebisho baadhi ya sheria ili kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa wawekezaji pamoja na ujenzi wa mitaa ya viwanda na jitihadi nyingine nyingi zinazochukuliwa na Mheshimiwa Rais zina lengo la kuhakikisha Tanzania inapiga hatua za haraka katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Kuhusu uhakika wa soko na usafirishaji wa bidhaa na malighafi Waziri Mkumbo amewatoa wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa Bandari ya Dar es Salaam pamoja na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali inayofanywa na Serikali inalenga kuhakikisha usafirishaji bidhaa ndani na nje ya nchi kwa haraka na uhakika.
Post A Comment: