Na Mwandishi wetu ,Morogoro


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameshiriki mkutano wa Baraza la Maji Afrika uliohusisha nchi zaidi ya hamsini.

Lengo la mkutano huo ni kushirikiana na nchi nyingine ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya maji, pia kulinda vyanzo vya maji ikiwemo mito na maziwa katika nchi hizo.

Akizungumzia mkutano huo  uliofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Mhandisi ,Mahundi amesema mkutano huo una manufaa makubwa kwa nchi kwani unawezesha kujenga mahusiano mema na mataifa mengine na hata kuwezesha kupata fedha za kutekeleza miradi ya maji.

Amempongeza Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliyechaguliwa  kuwa Mwenyekiti mwenza huku akitoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa uadilfu ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kuidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.


Share To:

Post A Comment: