NA Mwandishi Wetu – Moshi
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imejipanga kimkakati kupitia mpango kambambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2018, kukabiliana na athari na madhara yatokanayo na mabadiliko ya Tabia nchi katika sekta ya Kilimo.
Hayo yamesemwa leo mjini Moshi katika maonesho yanayoendelea kuelekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani na Mhandisi Naomi Mcharo, kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mhandisi Naomi amesema kuwa,mabadiliko ya tabianchi yamesababisha ukame na wakati mwingine mafuriko yanayosababisha madhara katika mashamba na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji, “ kwa hivyo sisi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tuna Mpango kabambe ambao tumeanisha kuanzia miaka 10 mpaka 20 ya kukabiliana na mabadilio ya Tabia nchi, kwa maana ya kwamba tumepanga kuwa na Ujenzi wa mabwawa nchi nzima takribani mabwawa 88, ambayo yapo kimakakati katika maeneo kame.” Alisisitiza.
Aidha, Mhandisi alibainisha kuwa mabwawa hayo yatajengwa katika maeneo ambayo yanapata ukame kwa muda mrefu na mvua zenye kuleta madhara.
Alibainisha kuwa, maeneo mbayo yatajengwa na yamejengwa mabwawa hayo kama vile katika wilaya ya Kwimba yanasaidia kukabiliana na athari na madhara yatokano na mabadiliko ya Tabia nchi.
Awali Mhandisi Naomi alieleza kuwa, Fedha zinazoingia katika mfuko wa Taifa wa Umwagiliaji zinatoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato, ikiwa ni pamoja na ukodishwaji wa mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ambapo fedha hizo zinatumika katika kazi ya matunzo, matengenezo na ujenzi wa Miundombinu katika skimu za kilimo cha umwaguliaji nchini, akitolea mfano wa ukarabati wa skimu ya Pawaga, na Dakawa unaoendelea, Ruaha Mbuyuni ambapo ukarabati wa kingo ya mto Lukosi ulioacha njia umekamilika, na Urumwi Ujenzi unaendelea wa mfumo shirikishi kwa wananchi yaani force account.
Post A Comment: