Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Rais Mstaafu mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kupiga hatua katika usawa wa jinsia kwa wahitimu chuoni hapo mwaka huu wa masomo 2021.
Pongezi hizo amezitoa wakati akiwatunuku Shahada za Kwanza wanafunzi wapatao 4,298 wa UDSM Kati yao, wanawake ni 1,973 sawa na asilimia 45.9 ambapo amefurahishwa
na idadi ya wanafunzi wa kike kuongezeka mwaka hadi mwaka na kuutaka
uongozi wa UDSM kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa wahitimu unafikia
asilimia 50 kwa 50.
"Nimesikiliza
hotuba yako Makamu mkuu wa chuo nimefurahishwa na takwimu kwamba
wahitimu wote wapo 4121 lakini kati ya wanaume ni 2101 na wanawake i
1920, hatua hii ni nzuri sana, usawa wa kijinsia kwa wahitimu wa shahada
za awali unaonekana kupanda hivyo nawapongeza sana kwa hatua hiyo,"
alisema Dkt. Kikwete.
Awali
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr. William Anangisye amesema kwamba chuo
hicho kimepata mafanikio makumbwa ikiwemo kupata kiasi cha Billioni 3
kwa ajili ya kufanya utafiti na ubunifu,pamoja nakuanza kudahili
wanafunzi kutoka mataifa yakigeni kwa ajili yakujifunza lugha ya
kiswahili.
Hata
hivyo Profesa Anangisye amewaasa wahitimu hao Kuwajibika kwa kutumia
elimu zao kuwa na ushawishi wa kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa
na Dunia kwa ujumla, kufanya kazi kwa bidii, pamoja na kuendelea
kujifunza mambo mapya na sio kubaki nyuma.
"Tuna
wapongeza sana mnaohitimu leo, lakini napenda niwakumbushe msiende
kutegemea kuajiriwa serikalini,bali mkawe chachu yakutengeneza ajira,
mfanye kazi kwa bidii, muwe na nidhamu kazini, mjiendeleze kimaarifa
lakini pia mkipata nafasi za kazi za kujitolea mfanye ili mjijengee
uzoefu nankujiami, kwahiyo msikate tamaa mnapokumbana na changamoto
mbalimbali za kazi" amewaasa Profes huyo
Nae
Mwayekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) Jaji
Mstaafu Damian Lubuva ameshukuru hatua zinazo chukuliwa na Rais Samia
kujikinga na uginjwa wa Uviko 19, nakutumia fursa hiyo kusema kuwa chuo
kinaendelea kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.
"Nyinyi
wahitimu na wale mnaobakia nawaomba muendelee kuchukua tahadhali kama
tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa uviko 19, rais
amekuwa mstari wa mbele kutukumbusha haya na sisi tuendelee kumuunga
mkono" amesema Jaji Mstaafu Lubuva.
Jumla
ya wahitimu 4121 wanahitimu katika ngazi ya cheti Shahada na
Astashahada katika mahafali ya 51 ya Chuo kikuu cha Dar es salaam
yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jiijini Dar es salaam.
Post A Comment: