Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Serengeti katika ziara ya Mawaziri 8 wa Kisekta iliyofanyika kijiji cha Busarara leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(kulia) akifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri 8 ya Kisekta , Mhe. William Lukuvi (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Serengeti katika kijiji cha Busarara leo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Chande akifuatiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb)
Watendaji wa serikali mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Serengeti katika ziara ya Mawaziri 8 wa Kisekta iliyofanyika kijiji cha Busarara leo.
*************************
Na Mwandishi wetu-Mara
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itaendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika vijiji saba vinavyoizunguka hifadhi hiyo ili kuinua uchumi wa wananchi wanaoshi katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo kwenye ziara ya Mawaziri 8 wa Kisekta leo.
Amesema kuwa kutokana na wananchi wa vijiji hivyo kutunza vizuri hifadhi hiyo, Serikali itaendelea kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Mwaka huu wa fedha tumetenga fedha za ujenzi wa madarasa mawili katika kijiji cha Kisangula, nyumba mbili za waganga na bwawa la kunyweshea mifugo katika kijiji cha Nyansulula na ukarabati wa bwawa katika eneo la Machocho". Amesema Mhe.Mary.
Pia, Mhe. Mary ameongeza kuwa Serikali itajenga kituo cha afya , nyumba za waganga na madarasa mawili katika kijiji cha Mbalibali, nyumba za waganga mbili, katika kijiji cha Tamkeni, madarasa mawili katika kijiji cha Nyambuli na kituo cha afya katika kijiji cha Bisarara Wilaya ya Serengeti”
Mhe. Masanja ameendelea kusisitiza kwa wananchi kutunza mazingira na kuitunza hifadhi hiyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Naye, Verpnica Nyamuhanga Mkazi wa Kijiji cha Bisarara amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuituma kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta kutembelea Serengeti kusikiliza wananchi na kutatua migogoro ya ardhi.
“Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa uamuzi wa kutuma mawaziri hawa na tunamuombea afya kwa Mungu ili azidi kufanya kazi zake vizuri zaidi” ameongeza Bi. Veronica.
Mhe. Mary yuko Mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta yenye lengo la kutatua changamoto za ardhi.
Post A Comment: