Na John Walter -Babati 

Michuano ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini na Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Paulina Gekul imeanza kutimua vumbi  katika ngazi ya Jimbo kwa Bodaboda kuwatandika wenzao waendesha Bajaji mabao 4-1 katika dimba la Kwaraa.

Michuano hiyo ambayo ilianza katika ngazi ya mitaa na Kata Oktoba 1,2021 imeanza kurindima katika ngazi ya Jimbo huku kata nane za jimbo hilo zikishiriki.

Gekul amesema lengo la mashindano  hayo ni kuinua vipaji vya michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa riadha,Netiboli na soka.

Mamia ya watu wamefurika katika uwanja huo kwenye michuano hiyo huku wadhamini mbalimbali wakijitokeza katika kufanikisha ligi hiyo ya Mbunge.

Mnunge huyo amekabidhi Mipira na vifaa vingine vya Michezo  katika shule mbalimbali za Sekiondari zilizopo katika jimbo hilo pamoja na timu zote za mitaa.


Share To:

Teddy Kilanga

Post A Comment: