Jane Edward,Arusha


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Peter Mathuki amefungua maonesho ya kwanza ya utalii kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, huku akishauri kuondolewa vikwazo vya kufanya utalii wa ndani baina ya nchi hizo.

Dk Mathuki ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya utalii nchi za Afrika ya Mashariki


Amesema kuwa nchi hizo zina weza kufanya vizuri zaidi kuhamasisha Utalii wa ndani kama vikiwa na viwango rafiki Kwa nchi zote.



Amesema maonesho hayo ambayo yanaendelea hadi Oktoba 11 katika viwanja vya TGT yameandaliwa vizuri na Serikali ya Tanzania licha ya kupata muda mfupi kujiandaa.



Kwa upande wake Waziri wa Maliasili, Dk Damas Ndumbaro amesema kufanyika maonyesho hayo ni  kunatokana na kuzinduliwa hivi karibuni mpango wa pamoja kutangaza utalii katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.


"Mwanzo huu ni mzuri na ni matumaini yangu nchi hizi zitafika mbali pamoja na kubadilishana uzoefu" Alisema Ndumbaro



Maonesho hayo yanatarajiwa kushirikisha Wadau wa Utalii kutoka mataifa 15 barani Afrika ambapo bidhaa na huduma mbalimbali za utalii zinaoneshwa.

Share To:

Post A Comment: