Katibu Mkuu wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiwavisha medali washindi wa riadha kwenye fainali za Mashindano ya Riadha ya Taifa jijini Arusha leo Oktoba 9, 2021
Katibu Mkuu wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (mwenye miwani) akiwa na viongozi mbalimbali wa michezo nchini, nyuma ni washindi wa riadha katika mashindano hayo
Wanariadha wa mbio za mita 10000 kwa wavulana
wakishindana leo Oktoba 9, 2021 jijini Arusha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan
Abbasi, ametoa medali mbalimbali jijini Arusha leo Jumamosi, Oktoba 9,
2021, kwenye kilele cha Michezo ya Riadha Kitaifa, akisisitiza kuwa
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ina jambo na
sekta ya michezo.
“Rais Samia ana jambo katika sekta ya michezo;
Serikali yake inawekeza sana katika michezo kama sekta ya kimkakati
kiuchumi, afya na utalii. Ndio maana ameongeza fedha za Timu za Taifa,
ametoa asilimia 5 ya mapato ya michezo ya kubashiri matokeo kusaidia
michezo na mwaka huu tunakwenda kurejesha Taifa Cup ambapo michezo
itachezwa kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa na kuja kifaifa. Uwekezaji
huu umeanza kuleta tija michezoni. Tuwe wamoja tu,” alisema Dkt. Abbasi.
Ametumia
fursa hiyo pia kuzitakia kheri na kuzipongeza timu mbalimbali za
Tanzania ambazo wiki hii na leo zinacheza/zimetwaa ubingwa wa aina
mbalimbali; Twiga Stars na Tanzanite Ladies(U20) leo zinashuka dimbani
Twiga ikiwania ubingwa katika fainali za COSAFA kule Afrika Kusini na
Tanzanite ikicheza na Eritrea Dar kuwania kufuzu fainali za kombe la
dunia.
Ameitakia kheri Taifa Stars inayoshuka uwanjani kesho
nchini Benin na ameipongeza Timu ya Taifa ya Kriketi U19 ambayo imeshika
nafasi ya tatu Afrika katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika juzi
nchini Rwanda.
Post A Comment: