Na Mwandishi wetu ,Mbarali
DIWANI wa kata ya Kongolo Mswiswi wilayani Mbarali Mkoani Mbeya ,Elia Bange amekabidhi vifaa vya shule aina ya printer na computer kwa ajili ya kuboresha elimu katika kata hiyo .
Diwani Bange amesema kuwa kadri anavyopata fedha ataendelea kusaidia mahitaji mbali mbali katika kata hiyo ambayo ina uhitaji wa vifaa hivyo ili kuwapunguzia adha ya kutembea walimu kutafuta huduma hiyo na badala yake muda huo utumike kufundisha watoto darasani.
“Leo hii nimekabidhi printer na computer katika shule ya msingi Azimio Mswiswi nawashukuru sana wadau wangu akiwemo Naibu waziri wa maji Mhandisi ,Maryprisca Mahundi (Mb)kwa kuniunga mkono na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi “amesema Diwani Bange.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Azimio ,Omary Mwambela alipongeza jambo kubwa lilofanywa na Diwani huyo na kuwataka waau wengine kusaidia shughuli za maendeleo katika kata hiyo .
“Kwenye hii kata tuna vitu vingi vya kusaidia tunaomba diwani wetu aungwe mkono kwa jitihada hizi anazofanya za kuboresha sekta ya elimu katika kata hii ,hii inasaidia walimu badala ya kuhaingika sasa mua huo watatumia kukaa kufundisha watoto wetu”amesema mwananchi huyo.
Post A Comment: