Raisa Said, Lushoto

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro amesema Wilaya hiyo imetengewa kiasi cha fedha sh.3.4 Bilioni za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Hayo aliyasema wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kisiwani na Kata ya Mayo katika Halmashauri ya Bumbuli ambapo alisema Fedha hizo ni sehemu ya 1.3 trilion zilizotolewa na serikali hivi karibuni

Mkuu huyo wa Wilaya alisema fedha hizo walizotengewa zinakwenda kumaliza changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madarasa,nyumba za Walimu na hivyo kufanya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha Kwanza kuondokana na changamoto hiyo.

"Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutupatia wana Lushoto fedha hizo. kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi, Ununuzi wa Mashine za Mionzi (X - Ray), Elimu Msingi - Elimu Maalum, Vyumba vya Madarasa katika Vituo Shikizi, Vyumba vya Madarasa katika Shule za Sekondari na Miradi ya Maji katika Kata za Mayo halmashauri Bumbuli" Alisema Kalisti.

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo alisema kwenye Ujenzi wa nyumba za Watumishi Halmashauri ya Bumbuli na Lushoto kila moja imepatiwa shilingi milioni 90 .

Kwenye Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imepatiwa Vyumba 54 vya Madarasa kwa shilingi Milion 20 kwa chumba kimoja hivyo kufanya Jumla ya shilingi 1,080,000,000/= na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imepatiwa Vyumba 27 vya Madara ambapo Kila chumba kimoja kimetengewa milion 20,000,000/=hivyo kufanya jumla ya sh milion 540,000,000/= ambapo gharama za Ujenzi wa Vyumba vyote vya Madarasa zitajumuisha pamoja na Ununuzi wa Viti na Meza.

Pia katika Elimu Msingi -Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum/Elimu Maalum wilaya imepokea jumla ya shilingi Milion 80,000,000/= kwa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto pia imetengewa fedha za Ujenzi wa Miundombinu ya Vyumba vya Madarasa katika Vituo Shikizi vya Shule kiasi cha Tsh 500,000,000/= kwa Ujenzi wa Vituo Shikizi 10 na Vyumba vya Madarasa 25.

Lazaro alisisitiza kuwa Bumbuli imepata fedha kiasi cha shilingi 420,000,000/= kwa ajili ya Ununuzi wa Mashine za Mionzi (X-Ray) katika Hospitali ya Wilaya hiyo na

Miradi Miwili ya Maji katika Kata za Mayo - Halmashauri hiyo Bumbuli ambao umepata milion 300,000,000/= na Kata ya Lushoto - Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ambao umepata mgao wa Fedha Tsh 300,000,000/=

kutokana na Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu kuzungumzia juzi kuhusu kutengwa kwa fedha hizo kumepelekea Mkuu wa Wilaya hiyo kusitisha ziara yake iliyokuwa inaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli ili kutoa nafasi kwa Wataalamu/Wakuu wa Idara wa Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani kuanza vikao vya Utekelezaji wa Maagizo na Maelekezo ya Serikali mara moja kwa Kuunda Kamati ya Uratibu na Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi.

"Nataka Utekelezaji wa Miradi uanze ndani ya Wiki mbili (siku 14) mara baada ya Fedha kupokelewa na Kuhakikisha Miradi ya Ujenzi wa Madarasa inakamilika kabla kuingia mwezi Januari 2022 na Miradi mingine ikamilike kabla ya tarehe march 30 mwkani.

Hata hivyo katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo Ramadhani Mahanyu amewataka Wataalam kuhakikisha wanasimamia fedha hizo vizuri ili wawe mikono Kwakuwa atakayetumia kinyuma hata kuwa salama.

Afisa Elimu Sekondari wilayani Lushoto Emmanuel Ebeneza alisema kuwa tunaishukuru sana Serikali kwa kutatua changamoto hii ya miundo

mbinu ya vyumba vya madarasa kwa Shule za Halmashauri yetu na kwa nchi nzima,watajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha matumizi ya fedha hizi yanaleta mabadiliko chanya katika kuondoa kabisa msongamano wa Wanafunzi darasani na kuleta tija katika zoezi zima la ufundishaji na ujifunzaji.
Share To:

Post A Comment: