Julieth Ngarabali, Kibaha.
Mkazi wa Visiga mjini Kibaha Mkoani Pwani Abdul Selemani (27) mfanyabiashara wa stetionary anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa la kutengeneza na kuuza nyara za Serikali ambavyo ni vitambulisho vya Taifa vya NIDA kinyume na sheria za nchi.
Kamanda wa Polisi Pwani Wankyo Nyigesa amesema oktoba 15 mjini Kibaha kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 12 saa 11 jioni huko Visiga kwa Kipofu mjini humo kwa kosa hilo.
Amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitengeneza vitambulisho hivyo na kuwauzia watu kwa sh. 10,000 kwa kila mmoja hali ambayo si salama kwa sababu anaweza hata kuwauzia raia wa nje ya nchi ama wahamiaji haramu na mwishowe nao kuonekana ni raia halisi kwenye maeneo mbalimbali.
"Huyu tunamshikilia kwa mahojiano zaidi kwa sababu tumemkuta anatengeneza vitambusho vya NIDA huku yeye sio muhusika, na amekuwa anaviuza kimoja sh, 10,000 , mtu yeyote aliyemfata na kuhitaji alitakia kulipa na kisha kutengezewa utaratibu ambao si salama kabisa maana anaweza kuwapa pia raia wa nje ama wahamiaji haramu "amesema Nyigesa
Kamanda huyo amebaisha kuwa mtuhumiwa huyo pia amekutwa na vifaa mbalimbali alivyokua anavitumia kuzalisha vitambulisho hivyo ikowemo Computa mpakato moja, PVC Card, kompyuta ya mezani (desktop ) , monitor, frash disk na printer.
Nyigesa ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post A Comment: