Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo (wa kushoto) akiteta jambo na Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kaskazini, Arnold Mapinduzi (wa kulia) walipofika katika Kiwanda cha Sayona, KIBOKO kinachotengeneza Plastiki, Rangi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo (aliyevaa Shati Jani la Mgomba) akitoa maelekezo wa baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Cocacola Tanzania kilichopo Mwenge, Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo
ametoa miezi Sita kwa Kiwanda cha Sayona Drinks Ltd kuhakikisha bidhaa
zake zinatafutiwa uhifadhi mzuri na hazichanganywi na bidhaa nyingine
zozote ili kuwalinda kiafya Watumiaji wa vinywaji hivyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mkoani
Dar es Salaam, akiwa kwenye Kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo
Mikocheni, Waziri Jafo amesema wanafanya maamuzi hayo ili kuwalinda
Watanzania kutumia bidhaa mbalimbali za Viwandani zikiwa salama bila
kusababisha athari kwao.
Waziri Jafo amesema katika Kiwanda hicho
cha Sayona amekutana pia na Kiwanda cha KIBOKO ambacho kinazalisha
bidhaa za Plastiki, yakiwemo Matanki sambamba na Rangi za Nyumba hali
inayohatarisha afya za Watumiaji wa kinywaji hicho kutokana n
kuchanganywa na bidhaa nyingine katika uhifadhi wake.
“Natoa
miezi Sita kwa kinywaji cha Sayona kitafutiwe sehemu yake na
kisichanganywe na bidhaa nyingine katika kuhifadhi”, amesema Jafo
Pia
Waziri Jafo amefurahishwa na kuwapongeza Kampuni ya Cocacola Tanzania
kusimamia vizuri mazingira yake kuanzia uzalishaji wa kinywaji hicho
katika kuhakikisha mifumo ya maji taka yanakuwa sehemu yake bila
kusambaa kiholela na kuleta madhara kwa jamii.
Post A Comment: