Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (katikati) akizungumza na watumishi wa TBS ambao wanahusika na ukaguzi wa magari bandarini mara baada ya kutembelea bandari katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujiona shughuli hiyo ikifanyika.

  1. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akiangalia namna zoezi la ukaguzi wa magari bandarini unafanyika baada ya kutembelea bandari katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujionea shughuli hiyo ikifanyika.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya mara baada kutembelea bandarini katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujionea shughuli hiyo ikifanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo mara baada ya Waziri huyo kutembelea bandarini katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujionea shughuli hiyo ikifanyika.

Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje TBS, Mhandisi Saidi Mkwawa akizungumza mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo mara baada ya Waziri huyo kutembelea bandarini katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujionea shughuli hiyo ikifanyika.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kipindi cha mwezi Aprili hadi kufikia Agosti 3, 2021 Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekusanya takribani Shilingi Bilioni 3.9 katika zoezi la ukaguzi wa magari bandarini yanayotoka nje ya nchi na kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.7 ambayo mwanzo ilikuwa inabaki nje kabla ya zoezi hilo kuanza kufanyika hapa nchini.

Ameyasema hayo leo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo mara baada ya kutembelea bandari katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujionea shughuli hiyo ikifanyika.

Amesema mpaka kufikia Agosti 3, 2021 TBS ilifanikiwa kukagua magari 11079 na katika magari hayo 7700 yalikuwa yamekidhi ubora na magari yaliyobaki yalikwenda kutengenezwa na baada ya kutengenezwa magari 1890 yaliweza kukidhi ubora na mengine yaliyobaki yapo gereji yakiendelea kurekebishwa.

"Kwa kuamua kutekeleza mpango huu, Serikali inaokoa fedha nyingi ambazo zingebaki nje hivyo kwa kipindi cha miezi mitatu tumekusanya takribani Bilioni 3.9 na fedha hii inaingia katika mfuko mkuu wa Serikali". Amesema Prof.Mkumbo.

Aidha Prof.Mkumbo ametoa wito kwa waingizaji wa magari nje ya nchi kushirikiana ipasavyo na TBS ili zoezi liweze kwenda vizuri hasa kuendelea kuelezea changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza ili waweze kuzitatua.

Pamoja na hayo Prof.Mkumbo ameipongeza TBS kwa juhudi ambazo wanazifanya katika mpango wa ukaguzi wa magari bandarini.

Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje TBS, Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kuna magari 1890 hayakufaulu kwenye hatua ya awali yanahitaji marekebisho ya taa, matairi na mengineyo, na hili lote limekuwa likiwanufaisha Watanzania kwasababu yanakwenda katika gereji ambazo Watanzania wanazimiliki .

"Bado dhamira yetu na jukumu letu la kukuza biashara inafanyika na tumeamua kufanya kazi hii kwa weledi lakini kikubwa kituo hiki kuanzia wiki ijayo tunaanza kujenga kituo kikubwa Cha kudumu ambacho kitakuwa na uwezo wa kupima vitu vingi na kukagua magari mengi". Amesema Mhandisi Mkwawa.

Katika utaratibu wa zamani ambapo ukaguzi wa magari kwa kiasi kikubwa ulikuwa unafanyika nje ya nchi na TBS kwa niaba ya Serikali tungepata asilimia 30% tu za fedha peke yake na asilimia 70% ingebaki nje.

[05/08, 15:12] Mbwilo Fullshangwe blog: TBS YAOKOA TAKRIBANI BILIONI 2.7 KATIKA ZOEZI LA UKAGUZI WA MAGARI
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: