Mbunge
wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi akizungumza na wananchi wa Kata ya
Chisano alipofika katika kata hiyo kuzungumza na wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akiwa amefika kwenye eneo ambalo limetengwa mahususi kwa ajili ya Kituo kidogo cha Treni ya Reli ya Tazara kilichopo Kata ya Chisano jimboni kwake.
Charles James,
SERIKALI
imejibu maombi ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi
juu ya kufunguliwa kwa kituo kidogo cha abiria kusubiri Treni 'Hot
Station' katika Kata ya Chisano kilichokuepo hapo awali lakini baadaye
kikafungwa lakini sasa serikali imeruhusu kiwepo.
Katika ziara
yake ya kikazi aliyoifanya Februari Mwaka huu, Mbunge Kunambi
alilalamikiwa na wananchi wake juu ya adha wanayoipata ya kushindwa
kutumia kituo hicho kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa Treni.
Akichangia
hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mei 18, Mwaka huu,
Kunambi alimuomba Waziri Dk Leonard Chamurilo kuruhusu kuwepo Kwa kituo
hicho kidogo ambacho kilifungwa kwa miaka 10 na hivyo kuwa changamoto
kwa wananchi wa Kata hiyo ambayo ni watumiaji wakubwa wa Reli hiyo ya
Tazara.
"Mlinipa changamoto ya Kituo kidogo Cha Treni hapa,
tunashukuru Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kukubali maombi yetu na sasa kibao kinachoashiria kuwepo kwa kituo
kimeshawekwa na kuanzia Mwezi ujao tunaamini Treni itakua inasimama
hapa.
Nyinyi ni mashahidi kwa miaka 10 kituo hiki kilifungwa
hivyo sasa kufunguliwa kwake ni msaada mkubwa kwetu kwani usafiri wetu
wananchi wa Chisano ni Treni, niwaahidi kama Mbunge wenu nitahakikisha
ndani ya muda mfupi anajenga choo na banda la kukuzuia mvua.
"
Baada ya Serikali kuturudishia kituo chetu hiki mimi kama Mbunge wenu
mnanidai Choo na Banda la kujizuia na mvua au jua ili pia kutoa fursa
kwa wajasiriamali kufanya biashara zao eneo hili na kuongeza vipato
vyao," Amesema Kunambi.
Kunambi amewaeleza wananchi wa Kata hiyo
ya Chisano kuwa tayari amepata kiasi cha Sh Bilioni 1.5 kwa ajili ya
kutengeneza miundombinu ya Barabarani kwenye Jimbo hilo na Kata hiyo
itanufaika na fedha hizo ambapo barabara zake nne zimetengewa fedha kwa
ajili ya kutengenezwa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata y Chisano,
Evaristo Danda amemshukuru Mbunge Kunambi kwa namna ambavyo amekua
akisukuma miradi ya maendeleo kwenye kata hiyo ikiwemo kufanikisha
kupatikana kwa kituo hicho cha Hot Station ambacho kitachangia kukuza
uchumi wa wananchi wake pamoja na kugusa sekta ya afya, elimu na maji.
Post A Comment: