Na Lucas Raphael,Tabora
JESHI
LA polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu wakiwemo mume na
watoto wake wawili kwa kula njama za kuumua mama yao na mume kuumua
mkewe aliyetambulika kwa ajina la Maria Kishiwa baada ya mwanamke
huyo kuungua maradhi kwa muda mrefu waliona kero hivyo wakalazimaka
kummalizaia mbali mama huyo .
Akizungumza na waandishi wa habari
kamanda wa polisi mkoani Tabora Safia Jongo alisema kwamba tukio hilo
lilitokea agasti 3 mwaka huu Asubuhi katika kijiji cha Isalalo kata ya
Utwigu wilaya ya Nzega mkoani hapa .
Alisema kwamba chanzo ni
kuugua maradhi kwa muda mrefu na mbinu iliyotumika ni kumfanga kamba
shingoni na kumninginiza ili aonekane kuwa amejinyonga.
Alisema
kwamba Maria alikuwa amefariki akiwa amefungwa kamba shingoni huku
akininginia na kamba ikiwa imefungwa kwa kukazwa kwenye nguzo ya jiko
kitu ambacho marehemu hakuwa na nguvu kiasi hicho baada ya kuugua kwa
muda mrefu
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi alisema kwamba
baada ya kumninginiza marehemu waliacha kinu na kigoda bila kuanguka
chini ili kuonyesha kuwa ndipo alipopanda na kujinyoga .
“Wakati
ni vigumu kwa mtu mgonjwa kupanda hadi kuwe na masada wa watu wengine
jambo ambalo lilileta mashaka “ alisema kamanda Safia .
Alisema
kwamba marehemu Maria alikuwa analala na mjukuu wake ambaye alifichwa
ili asibaini mbinu hiyo ya mauaji jambo hilo ndilo lilipelekea polisi
kuanza kuchuguzi ambapo mjukuu huyo alisema kila kitu kilichofanyika
kumuua bibi yake.
Alisema kwamba majina ya watu hao watatu yamehifadhi kwa ajili ya uchuguzi mzima wa tukio hilo la kinyama
Hili
nituo la pili kutokea katika wilaya ya nzega kwa muda wa usiozidi wiki
Tatu baada ya watoto wawili wakiwa wanachunga mifugo kuuawa na kufukiwa
kwenye shimo ili kupoteza ushaidi.
Post A Comment: