Walimu na Wanafunzi wa shule ya
sekondari Soni day iliyopo Bumbuli Mkoani Tanga wamemshukuru Mbunge wao
January Makamba kwa kutimiza ahadi yake ya vitanda 20 vyenye thamani
ya mil.4.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi walisema
'hostel' ya shule yao iliungua mara mbili na tangu ikumbwe na kadhia
hiyo walikumbana na changamoto ya ukosefu wa vitanda hivo kulazimika
kulala chini kutokana na vitanda vilivyokuwepo kuungua wakati wajanga
hapo shuleni kwao.
Mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyefahamika
kwajina la Mashoo Mrema alisema kuwa msaada huo wa Mbunge umekuja
wakati muafaka wakati wao wakiwa na uhitaji wa vitanda hivyo.
Mrema
alisema kuwa pia vitanda hivyo vitawasaidia kuwapa nguvu ya kujisomea
na kuondokana na mawazo na magonjwa ya kukohoa waliyokuwa wanayapata
kutokana na kulala chini.
Ally Lwena ni Mkuu wa shule hiyoAlisema
Kwanza anampa shukrani Mbunge wao kwa Kusikia Kilio hicho Cha
vitandanda vya wanafunzi wa kike katika shule hiyo.
Lwena
alisema hatua hiyo itasaidia kupata wanafunzi wengi watakaokaa Hostel na
hivyo kuwaongezea Muda Mwingi Wakujisomea hatimaye Kuongeza Ufaulu wa
Shule Na Halmashauri kwa Ujumla.
Pia Mkuu huyo wa shule alieleza
kuwa kutokana na kukosekana kwa vitanda Wanafunzi walikuwa wakipigwa na
baridi kali iliyokuwa inatoka kwenye sakafu na kuwapata moja kwa moja
wanafunzi Ilisababisha magonjwa kama vile kukohoa , kubanwa na mbavu na
hata vichomi.
Kwa upande wake Mbunge Makamba alisema tangu
ameingia madarakani amekuwa akisadiana na wananchi wake kutatua
changamoto mbalimbali pamoja na kutekeleza ahadi anazoahidi.
Makamba
alisema wakati shule hiyo imekumbwa na kadhia ya janga la moto yeye
kama Mbunge alitoa fedha zake mfukoni na fedha kutoka kwa marafiki zake
waliweza kununu vitanda 100 na bati 200 nakwamba ahadi iliyokuwa imebaki
ni hiyo ya vitanda ambayo inakamilika Sasa.
Hata hivyo alieleza
kuwa lengo la kusaidia katika shule hiyo ni kutaka kuunga mkono
jitihada za kuinua kiwango Cha elimu na ufaulu katika jimbo lake.
Home
Unlabelled
"JANUARY MAKAMBA ATOA MSAADA WA VITANDA KWA WANAFUNZI VYENYE THAMAN YA Mil4"
Post A Comment: