Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Dk Suleiman Serera, amewataka
wanasiasa, viongozi na wananchi wa eneo hilo kuachana na siasa za
unaharakati na kugeukia siasa za maendeleo.
Dk
Serera ameyasema hayo alipotembelea na kukagua shule ya serikali ya
msingi ya Bilionea Saniniu Laizer ya mchepuo wa kiingereza iliyojengwa
na mchimbaji huyo maarufu wa madini ya Tanzanite.
Amesema
maendeleo ya wilaya ya Simanjiro hayatapatikana endapo kutakuwa na
siasa za uanaharakati badala ya kulenga kwenye malengo ya maendeleo
katika sekta mbalimbali.
Amesema
kila mmoja akiimba wimbo wa maendeleo watafika mbali kwa maendeleo ila
wakianza kuweka kipaumbele kwenye siasa hizo za uanaharakati hawatafika
popote.
“Mimi
nikiwa na kauli moja, mbunge akiwa na kauli moja, Mwenyekiti wa
halmashauri na madiwani tukiwa na kauli moja ya maendeleo tutaifikisha
mbali Simanjiro yetu,” amesema Dk Serera.
Mjumbe
wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Manyara, Kiria Laizer amesema baadhi
ya watu wasio na nia njema wamekuwa wanamkatisha tamaa bilionea Laizer
kwa maneno ya uzushi.
“Bilionea
Laizer amekuwa akisaidia jamii ila kumekuwa na wakatishaji tamaa
wanajenga hoja za fitina kwa lugha ambazo hawafanyi utafiti,
zinazorudisha nyuma maendelo,” amesema Laizer.
Bilionea
Laizer amesema shule hiyo imekuwa tumaini kwa jamii ya wafugaji na
wakulima wadogo ila wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa walimu.
“Nitajenga
bwalo la kulia chakula hivyo tunaiomba serikali ijenge bweni ili Esto
wa wafugaji na wakulima waweze kulala na tuwabane wasome na kusaidia
jamii baadae,” amesema bilionea Laizer.
Kaimu
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Silvanus
Tairo amesema shule hiyo ilianza kujengwa madarasa mawili na hivi sasa
imekamilisha madarasa yake.
“Tunampongeza
mdau wetu wa maendeleo bilionea Laizer ambaye ameacha alama kubwa kwa
kujenga shule hii ambayo ni ukombozi wa elimu kwani ni ya mfano kwa
mkoa,” amesema Tairo.
Post A Comment: