Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto)
akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza za walimu toka kwa Meneja wa
NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (kulia) hafla iliyofanyika
Shule ya Sekondari Mchikichini jana jijini Dar es Salaam. Katika hafla
hilo NMB ilikabidhi msaada wa Viti 190, meza 60 na Madawati 100 kwa
Shule za Sekondari Kipunguni na Mchikichini, pamoja na Shule ya Msingi
Kibaga zote za jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (wa nne kulia) pamoja na
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa tatu kulia)
wakimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania
(TAB), Bw. Omar Itambu sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye
thamani ya shilingi milioni 14 jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo
umetolewa na Benki ya NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi
wa NMB (kulia).Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omar Itambu
(mwenye kipaza sauti) akiishukuru Benki ya NMB mara baada ya kupokea
sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye thamani ya shilingi
milioni 14 jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Benki ya
NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa NMB (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto) akikabidhi sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye thamani ya shilingi milioni 14 kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omar Itambu na viongozi wa TAB jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa NMB (kulia).
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto)
akikata utepe kuzinduwa sehemu ya msaada wa viti na meza za walimu
zilizotolewa na Benki ya NMB kwa Shule za Sekondari Kipunguni na
Mchikichini, pamoja na Shule ya Msingi Kibaga zote za jijini Dar es
Salaam, kulia mwenye suti ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam,
Donatus Richard. Msaada huo uliotolewa jana na NMB unasamani ya shilingi
14,700,000/-.
Post A Comment: