Na. Angela Msimbira KIGOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mika na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia Mifumo ya kielekroniki katika ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri na kupelekwa benki ndani ya masaa 24
Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma leo kwenye ziara ya kufuatilia shughuli za maendeleo katika mkoa huo katika Sekta ya Afya ya msingi, maendeleo ya shule za msingi na Sekondari, mundombinu ya barabara na ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi ya Halmashauri.
Waziri Ummy amaeendelea kufafanua kuwa kila Halmashauri inawajibu wakuhakikisha wanatumia mifumo hiyo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha katika Halmashauri.
Ameendelea kufafanua kuwa Halmashauri zinatakiwa kuhakikisha mapato yanayokusanywa na Halmashauri yanaingizwa benki ndani ya masaa 24 kwa kuwa kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Kigoma, Halmashauri 6 zimepata hati zenye mashaka na Halmashauri 2 zimepata hati za kuridhisha katika mwaka 2019/2020 sababu kubwa ni fedha kukusanywa na kupelekwa kwa wakati benki.
Amezitaja Halmashauri ambazo zilikusanya fedha na kutokuzipeleka benki kwa wakati lakini kwenye mfumo yanaonekana kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo haikupeleka kiasi cha shilingi milioni 378, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu milioni 112 , Halmashauri ya Buhighwe milioni 74 na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo 430 na Halmashauri ya Wilaya wa uvinza shilingi milioni 318.
Amewataka Viongozi wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinapelekwa benki kwa wakati.
Aidha, amewaagiza viongozi hao kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na yanatumika katika kutatua kero za wananchi ambapo kila shilingi 100 inayokusanywa shilingi arobaini inatengwa kwa ajili ya kutatua kero za wananchi wa Kigoma.
Post A Comment: